Jinsi ushawishi wa Kaunda ulivyosukuma kukubalika kwa vyama vya upinzani barani Afrika
Jinsi ushawishi wa Kaunda ulivyosukuma kukubalika kwa vyama vya upinzani barani Afrika julai 2, 2021 Jumanne Juni 15, 2021 Afrika ilishtushwa na taarifa za kifo cha Rais wa kwanza wa Zambia Dk Kenneth Kaunda baada ya kulazwa hospitali akiuguwa homa ya mapafu. Amefariki akiwa na umri wa miaka 97. Dk Kaunda maarufu KK ameaga dunia akiacha swali ni kwa umbali gani alikuwa na ushawishi kwa mwandani wake, Rais wa Tanganyika na baadaye Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na kurejea mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini humo 1992? Mfumo wa vyama vingi Tanzania ulifutwa kufuatia marekebisho ya katiba ya mpito 1965 mwaka mmoja baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, hivyo kuwa na chama kimoja tu,Tanganyika African National Union (TANU). 1972, miaka minane baada ya uhuru, Zambia ikafuata njia hiyo hiyo na kubakia chama kimoja tu, chama tawala United National People´s Union (UNIP) Ulikuwa mtindo uliofuatwa takriban na mataifa mengi barani Afrika. Baada ya miongo kadhaa...