Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 8, 2023

Yanga vs Geita

Picha
 Hatua ya Robo Fainali Kombe la Azam Sports Federation kukamilika kupigwa leo  Saa 2:00 Usiku, mabingwa watetezi Yanga SC watakuwa uwanja wa Azam Complex wakiwakaribisha Geita Gold Je, Wachimba dhahabu kuwatupa nje wananchi ama ama Yanga kwenda nusu fainali kuungana na Singida Big Star, AzamFC na Simba??

Lampard arudi Chelsea kwa muda

Picha
Frank Lampard ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa Chelsea FC ambapo atainoa timu hiyo hadi mwisho mwa msimu. Lampard anarudi tena Darajani kama kocha baada ya kuitumikia kwa mafanikio akiwa mchezaji akishinda mara tatu Ligi Kuu ya England pamoja na taji moja la UEFA. Lampard ataongoza Chelsea katika mchezo wa robo fainali wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Aprili 2 mwaka huu Chelsea ilivunja mkataba na Graham Potter kutokana na matokeo yasiyorodhisha, na sasa itakuwa katika kibarua cha kutafuta kocha wa kudumu.