Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 21, 2023
 #SOMO la leo 20/08/2023 na Mtu wa MUNGU Nabii BG Malisa. ▪︎LUKA 19:29-30 Unaweza ukawa unaishi mahali flani lakini katika ulimwengu wa roho umefungwa kijijini kwenu. Kijiji chenu ndiyo chimbuko lenu, ndiyo asili yenu. Huwezi kufanikiwa zaidi ya asili ya kijiji chenu. ▪︎Kule ulipotoka ndiyo chimbuko lenu, ndipo historia yenu ilipo, huwezi kwenda zaidi ya chimbuko lenu, inahitaji ukombozi na kufunguliwa kwa kiwango cha juu ili ufanikiwe. Kumbuka: NI LAZIMA URUDI UCHUNGUZE ASILI YA KIJIJI CHENU NA UISHUGHULIKIE ▪︎Ardhi ya kijiji chenu inahitaji ukombozi wa hali ya juu, watu wengi wapo mjini wanapambana kutafuta mafanikio, wanatafuta upenyo na hakuna chochote kinachotokea, pasipo kujua kuwa msingi wa maisha yao unategemea kule walipotoka. Tambua na uelewe kwamba kuna siri kubwa iliyojificha katika ardhi ya kijijini kwenu. ▪︎MARKO 8:26. Kuna matatizo mengine yanatokana na maeneo ulipotoka, katika kijiji chenu kuna maagano yalifanyika yakakushikilia mpaka leo. Kuna matatizo mengine siyo...