Magonjwa ya macho
Magonjwa ya macho Jicho lenye conjunctivitis kutokana na virusi . Magonjwa ya Macho ni maradhi mbalimbali yanayoweza kuyapata macho . Jicho ni kiungo kimojawapo cha mwili kinachomsaidia mwanadamu na pia wanyama kuona vitu mbalimbali katika dunia na hata ulimwengu kwa jumla. Mnyama yeyote akikosa macho ni adhabu kubwa sana kwa maisha yake ambapo asipokuwa na mwangalizi anaweza kupata adha mbalimbali kama kukosa chakula na inaweza kumpelekea mnyama kufa kwa kukosa chakula kwa sababu haoni. Magonjwa ya macho yapo ya aina mbalimbali: mengine yanasababishwa na nzi , kama vile trakoma , na mengine yanasababishwa na mionzi ambayo inaweza kuwa ya jua , runinga na hata tarakilishi ambavyo vinasababisha macho kutofanya kazi vizuri kama kuona mbali na kuona karibu na pia kichwa kuuma . Makengesa katika macho yanasababishwa na kulegea kwa mishipa ya siliari inayoshika lenzi ya jicho. Magonjwa yote ya macho yanatibika; inategemea hatua ya ugonjwa huo wa macho ulipof...