Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 29, 2023

KUONGOZWA NA ROHO.

 KUONGOZWA NA ROHO. Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:- 1.      Afanye kazi, 2.      Awe na umiliki juu ya nchi, 3.      Azalishe, 4.      Aombe, 5.      Ashuhudie, 6.      Aabudu, 7.      Lazima awe mtoaji, 8.      Lazima uwe na upendo, penda uumbaji, 9.      Lazima asamehe na atubu, 10.  Ahakikishe anatunza wito wake. Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda, 1 Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” Mungu ametupa ufunuo kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini, maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo kuhusu wewe, Mungu au ya ibilisi yaliyo katika roho hiki ndicho tunakiita ufunuo inamaana yamefunuliwa kwako. Biblia inasema “Lakini Mungu ametufunul...

TUNDA LA ROHO

 Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria." - UPENDO  Hili ni tunda la kwanza la Roho, Yesu Kristo wakati akitembea watu wengi walimfuata kwasababu alikuwa na Pendo la kweli ambalo ni tunda lililosababisha watu kumfuata kila alipo pita, Pendo linamvuta mtu kuja karibu yako, hivyo katika kanisa ni lazima kuwa na tunda la upendo ili kusababisha ukombozi wa watu.  - FURAHA Furaha inajengwa na Pendo, kama kanisa furaha inasababisha umoja na ushirikiano na inasababisha ukombozi kwetu.  - AMANI Amani ni kila kitu katika maisha, pasipo amani hakuna mafanikio. Ndani ya amani kuna utoshelevu kwa kila jambo.  - UVUMILIVU Uvumilivu na tabia ya Mungu , kama Mungu wetu anaweza kutuvumilia na sisi pia tunapaswa kuwa wavumilivu kwa kila jambo - UTU WEMA Utu wema ni kuwaza mema juu ya mtu mwingine -FADHILI Fadhili ni ile hali ya kujitoa kwa ajili ya mtu Fulani pas...