Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 6, 2021

MIAMBA YA SOKA TZ sasa Yasubiriana Kigoma

Picha
  MIAMBA YA SOKA TZ sasa Yasubiriana Kigoma JULai 06 2021         BAADA ya Yanga juzi kuilaza Simba bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, mashabiki wa timu hizo jijini hapa wamesema watakutana Julai 25 huko Kigoma na mbabe atajulikana zaidi msimu huu. Katika mchezo wa juzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga iliichapa Simba na kufikisha pointi 70, ikiachwa alama tatu na wapinzani hao, huku ikiwa mbele kwa mechi mbili. Simba waliingia uwanjani wakihitaji ushindi ili kutangazwa mabingwa lakini Yanga walikuwa makini kuharibu mipango na kufanikiwa kupata bao mapema kupitia Zawadi Mauya na kufanya ligi kuendelea kuchangamka upande wa ubingwa. Baada ya mchezo huo wa ligi, timu hizo zinatarajia kukutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma. Sebastian Mwandala ambaye ni shabiki wa Yanga alisema timu yao haiwezi kufungwa na Simba na kwamba hizo ni salamu kuelek...

mtanikuta Kigoma MZEE MPILI

Picha
mtanikuta Kigoma MZEE MPILI JULai 06 2021         SIMBA wanalia wakiwaambia wababe wao Yanga kwamba mumshukuru Mzee wenu Mpili vinginevyo mngekula nyingi lakini mwenyewe amejibu mapigo akiwaambia ‘Hapo mmepigwa na nyuklia moja tu mmesambaratika sasa subirini Kigoma mi natangulia’. Yanga ilicheza kwa mbinu bora zaidi dhidi ya Simba juzi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 la mapema dakika ya 11 tu kutoka kwa kiungo Zawadi Mauya na kuwacheleweshea Wekundu hao sherehe za ubingwa wa nne mfululizo. Akizungumza jana na Mwanaspoti, Mzee Mpili ambaye ni shabiki wa Yanga kutoka Ikwiriri, Pwani alisema watani wao wana bahati kwani walikuwa wapigwe nyingi katika mchezo wa juzi. Mzee Mpili ambaye alionekana kuwa mwenye furaha akiwa amevaa fulana yake safi akaenda mbali akisema safari ya kuipiga Simba ndio imeanza na sasa anatangulia mkoani Kigoma kuanza maandalizi ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) utakaochezwa Julai 25 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika. “Sim...