Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 13.07.2021
Manchester United wako mbioni kukubaliana masharti binafsi na mlinzi wa Real Madrid Raphael Varane,27, ambaye amekuwa akitolewa macho kwa muda mrefu.(Daily Mail) Hector Bellerin ameiambia Arsenal kuwa anataka kuondoka wakati wa dirisha la usajili majira ya joto. Mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi mwenye miaka 26, ambaye ni mchezaji wa muda mrefu wa kikosi cha kwanza cha Mikel Arteta ana matumaini ya kuhamia Inter Milan. (Metro) Manchester City haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Antoine Griezmann, 30, lakini wana nia na mshambuliaji wa Norway na Borussia Dotmund Erling Braut Haaland, 20, na nahodha wa Tottenham England Harry Kane. (The Sun) Chelsea inatarajia kutangaza 'ofa kubwa' kwa Haaland. (Daily Star) Griezman anaweza kuelekea kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid, kwa kubadilishana na kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez,26. (Daily Express) Tweet ya kiungo wa kati wa Real Madrid Isco -iliyofutwa - inadokeza kwamba mch...