Nguvu ya Mwamini.
Nguvu ya Mwamini. 2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” Hauhitaji kukumbuka ya jana kwa maana yamekwisha, ni kwa nini haupokei kutoka Mungu? ni kwa sababu wewe unawaza ya jana. Mungu hana mpango wa jana yako, kwa nini? Kwa sababu jana ni ya kale na imepita, Mungu anampango na nini? Mungu anampango na leo na kesho yako, Mungu ana shauku mno na kesho yako, kama unataka kutembea na Yeye zingatia mapenzi yake, mapenzi yake sio jana yako bali mapenzi yake yapo katika kesho yako. Kama upo ndani ya Kristo na umezaliwa mara ya pili yaani umeokoka Mungu anashauku sana na wewe, anasema jana yako imepita. Jana ni mambo ya kale, je ni nani anaye zingatia mambo ya kale? Tunatumia vitu vya kale kwa ajili ya kuvitazama tu tunaenda katika makumbusho ili kuona vitu vya zamani tu, hauzingatii sana vitu vya kale. Kwa nini unampango sana na jana yako wakati jana yako imepita, ilihali hata nguo zako za j...