WAABUDUO
SOMO: WAABUDUO Mwanzo 1:1-2 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.” Hapo mwanzo tunamuona Mungu akiumba mbingu na nchi, yapasa tufahamu nadharia yetu ya ibada, nadharia yetu ni nini? Ni mwanzo, tukiufahamu mwanzo basi tunaweza kuabudu katika uhalisia wa Ibada. Biblia inasema hapo mwanzo Mungu, si Efatha, Josephat wala waabuduo bali hapo mwanzo tunamuona Mungu akifanya kazi ya uumbaji. Alichokiumba kilikuwa ni kitupu na kikiwa, hii inamaana kuwa hicho alichokiumba Mungu kilikuwa kinahitaji utimilifu. Mwanzo 1:3 “ Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.” Hapa tunagundua ibada ni Nuru, hii inamaana gani? Utimilifu, na ukamilifu ni mzuri. Tunapoabudu yapasa tuanze mwanzo na tu...