Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 26, 2021

Rais wa Tunisia amemfukuza kazi waziri mkuu

Picha
Rais wa Tunisia amemfukuza kazi waziri mkuu kusitisha shughuli za bunge, kufuatia kuzuka kwa vurugu za maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana na kupambana na Polisi siku ya Jumapili kuonyesha hasira zao dhidi ya serikali kwa namna inavyoshughulika vibaya suala la Covid-19, Rais Kais Saied alitangaza atasimamia hilo kwa kusaidiwa na waziri mkuu mpya, akisema anataka kuleta utulivu nchini humo. Lakini wapinzani wake wanasema hatua aliyoichukua Rais huyo ni kama kupindua ama mapinduzi ya kimamlaka. "Tumechukua hatua hizi... mpaka hali ya Tunisia irejee kuwa shwari, mpaka tukiokoe nchi," alisema Saied katika hotuba yake kwenye televisheni baada ya kuitisha kikao cha dharura cha usalama. Usiku wa Jumapili, waandamamaji walilipuka kwa shangwe kufuatia taarifa kwamba waziri mkuu Hichem Mechichi ametimuliwa. Baadae Rais Saied akaungana na maelfu ya waandamamaji katika mji mkuu Tunis. Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana mjini Tunis na m...

aliye tumwa kuwakomboa watoto wa shule naye atekwa..

Picha
  Watekaji nyara nchini Nigeria wamemkamata mwanaume aliyetumwa kupeleka malipo ya fidia ili kuachiliwa kwa makumi ya watoto wa shule waliotekwa nyara. Mzee huyo alitumwa na wazazi wa watoto hao baada ya kufanikiwa kukusanya naira 30msawa na (dola 73,000; Pauni 53,000) kwa kuuza ardhi na mali zingine. Lakini wameachwa wakiwa hawana matumaini kufuatia utekaji nyara wake. Kaskazini mwa nchi hiyo kuna wimbi la utekaji nyara shuleni unaotekelezwa na wahalifu kwa ajili ya kujipatia faida. Mara nyingi katika matukio kama hayo fidia hulipwa lakini hii ni kesi nadra ambapo mtu aliyebeba pesa iliyokuwa fidia na kuwapelekea naye pia ametekwa nyara. Watekaji nyara walimpigia simu mwalimu mkuu wa shule na kusema kwamba pesa zilizotolewa sio kiwango walichokubaliana. Wanafunzi 136 walitekwa nyara kutoka shule ya Kiislamu huko Tegina, jimbo la Niger, mwishoni mwa Mei. Watu wenye bunduki waliokuwa wamepanda pikipiki walivamia mji huo na kuanza kufyatua risasi kiholela na kumuua mtu mmoja huku mwi...