SIMBA tayari imezindua Wiki ya Simba Day jijini Dar es Salaam, huku baadhi ya viongozi, wanachama pamoja na wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo wakijitolea kutoa damu kuchangia Mfuko wa Damu wa Taifa, huku mmoja ya wataalamu akimuonya nyota mpya Luis Miquissone. Luis amerejeshwa kikosini katika dirisha la usajili lililopo wazi kwa sasa na tayari ameanza mambo katika kambi ya timu hiyo iliyopo Uturuki, lakini kocha wa zamani wa timu hiyo ambaye kwa sasa kahamishia makali yake kikosi cha vijana cha Msimbazi, Seleman Matola amemtahadhari mapema. Kocha huyo wa vijana wa Simba, alisema licha ya Luis kuwa bado mchezaji nzuri, lakini anakibarua cha kufanya ili aweze kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo walio na matumaini makubwa Luis aliyeuzwa na Simba misimu miwili iliyopita kwa Al Ahly ya Misri na kuacha pengo kubwa katika kikosi hicho, amejereshwa baada ya kumaliza na mabosi wa klabu hiyo akipewa mkataba wa miaka mitatu na Matola aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho alisema kurudi k...