Rais wa Tunisia amemfukuza kazi waziri mkuu

Rais wa Tunisia amemfukuza kazi waziri mkuu kusitisha shughuli za bunge, kufuatia kuzuka kwa vurugu za maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana na kupambana na Polisi siku ya Jumapili kuonyesha hasira zao dhidi ya serikali kwa namna inavyoshughulika vibaya suala la Covid-19, Rais Kais Saied alitangaza atasimamia hilo kwa kusaidiwa na waziri mkuu mpya, akisema anataka kuleta utulivu nchini humo. Lakini wapinzani wake wanasema hatua aliyoichukua Rais huyo ni kama kupindua ama mapinduzi ya kimamlaka. "Tumechukua hatua hizi... mpaka hali ya Tunisia irejee kuwa shwari, mpaka tukiokoe nchi," alisema Saied katika hotuba yake kwenye televisheni baada ya kuitisha kikao cha dharura cha usalama. Usiku wa Jumapili, waandamamaji walilipuka kwa shangwe kufuatia taarifa kwamba waziri mkuu Hichem Mechichi ametimuliwa. Baadae Rais Saied akaungana na maelfu ya waandamamaji katika mji mkuu Tunis. Maelfu ya watu wamekuwa wakiandamana mjini Tunis na m...