MBUNIFU WA UMEME NA ZANA ZAKILIMO NJOMBE AFARIKI DUNIA

Njombe . Mamia ya wananchi wamejitokeza kushiriki maziko ya aliyekuwa mbunifu wa umeme na zana za kilimo mkoani Njombe, John Fute maarufu kama ‘Mzee Pwagu’ aliyefariki dunia Ijumaa, Julai 28, 2023. Mzee Pwagu ambaye alijipatia umarufu kutokana na kazi zake na kuitwa Ikulu na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli, ameagwa na kuzikwa leo nyumbani kwake mtaa wa Msete Halmashauri ya Mji wa Njombe. Wakizungumza kwa masikitiko leo Jumapili, Julai 30, 2023 wananchi walioshiriki mazishi ya Mzee Pwagu wamesema msiba huo ni mkubwa kwao kutokana na shughuli alizokuwa anazifanya zilikuwa na manufaa siyo tu kwa upande wake bali kwa jamii iliyomzunguka, mkoa na taifa kwa ujumla. Marehemu Mzee Pwagu wakati wa uhai wake alitengeneza umeme ambao unakadiriwa kuwa na killowatt 28 kwa ajili ya matumizi yake na majirani waliomzunguka. Kupitia utengenezaji wa pampu za umwagiliaji, marehemu atakumbukwa hasa na wakulima wa parachichi kwani aliwasaidia katika kuwezesha kilimo cha umwa...