POMBE NI ANGAMIZO LA UCHUMI TANZANIA

habari mpendwa msomaji wangu, leo nimeona nitoe uelewa wangu huu ili niwashirikishe jamii ya kitanzania, hasa wapenda maendeleo na wale wanao tamani kuiona Tanzania ikikua kiuchumi, kutoka hapa tulipo, yaani uchumi wa kati wa chini, Nakwenda uchumi wakati wa kati hadi juu. suala la kodi ni suala mtambuka sana, wengi wa wafanya biashara walipa kodi huwaona wadai kodi kama adui zao na warudishaji wa biashara zao nyuma, hii ni kutokana na aina au namna ya wakusanya kodi wanavyo wachukulia walipa kodi na namna wanavyo wafikia kudai kodi, kodi ni mhimu sana ili nchi iweze kufanya miundo mbinu itakayo rahisisha wafanya biashara hao hao kukuza na kuongeza mzunguko wa fedha katika biashara zao, pia kodi inawezesha kila mwananchi kupata mahitaji mhimu ya kila siku hii ni kwa watu wote wafanya biashara, wafanya kazi, wakulima n.k. sasa sitaki twende sana huko, acha tuone bajeti iliyo pita 2021-2022 leo naegemea katika kipengele kimoja cha kushusha kodi katika vileo na kupandisha katik...