UJUMBE WA ROHO.
Nalikuwa katika njozi NAMI nikaona tazama watu katika mji wangu wakienndelea na shughuli zao, Lakini wanadamu wote tunaonekana tunanamchukulia MUNGU YEHOVA na IBADA ZAKE kuwa kitu Cha kawaida, inaonekana hakuna injiri ya kweli Kwa wanadamu wa muda huo. Basi ilikuwa ni siku iliyo Anza vizuri sana, Jua la ASUBUHI liliangaza vyema bila kuwepo hata wingu Moja, Ilionekana hakuna mvua inaweza kunyesha siku hiyo. Watoto walikuwa wakienndelea na michezo Yao huku watu wazima wakiendelea na shughuli zao, GHAFRA ,. YAANI KUFUMBA NA KUFUMBUA milimani ikaonekana wingu na dhoruba Kali ambayo hapana mtu akikutwa nayo anaweza kupona, Dhoruba Kali ilikuwa inakuja mjini kwetu Kwa Kasi isiyowezekana kuikimbia. Watu wa mji walionekana wakikimbia kila mmoja aiokoe nafsi yake bila hata kuwakumbuka watoto wao na ndugu na jamaa zao. NAMI nilitaka kukimbia lakini nikawaona wanagu wadogo wakiwa wame duwaa Wanashangaa Ile tufani Kwa huzuni. Nikajiuliza inamaana hata mama Yao kwaacha? Basi nikaenda nik...