Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 30, 2021

KUFUNGA

  KUFUNGA: Nini maana ya kufunga? Isaya 58:6-14 “ Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde……. ” ·          Kufunga maana yake ni kuachilia matendo maovu. ·          Kufunga ni kukusababisha wewe kutimiza mapenzi ya Muumba wako, ·          Kufunga ni kumwambia Mungu mimi sistahili pasipo wewe, yaani inamaana ni kumkaribia Mungu. ·          Kufunga ni kuuita uwepo wa Mungu uwe pa...

NGUVU YA DAMU YA YESU

  NGUVU YA DAMU : Damu ya Yesu ndiyo inayomfanya mwamini awe mtakatifu wa Mungu, hauwi mtakatifu pasipo Damu ya Yesu kukusafisha. Unahitaji damu ya Yesu kukusafisha ili uwe mtakatifu wa Mungu. Haki huja kupitia Neno lakini utakatifu huja kwa kupitia damu. Katika damu ndipo ukombozi ulipo,  huwezi kutoka kwenye dhambi na uovu ambao unaokufanya usiwe mtakatifu pasipo Damu ya Yesu, ni kwa Damu pekee ndiyo itakufanya uwe mtakatifu wa Mungu na huo utakatifu ndio unamfanya Mungu avutiwe na wewe. Utakatifu wako ndio utakao mvutia Mungu lakini ili uupate ni lazima uipate Damu ya Yesu na hapo ndipo ukombozi ulipo. Nguvu inayo fukuza dhambi zote maradhi na magonjwa ni damu ya Yesu, kupitia Damu tunao ukombozi wetu, wokovu, utakatifu, tunakuwa washiriki wa mambo ya mbinguni. Ufunuo 12:11 “ Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa .” tunamshinda adui, maradhi na magonjwa kwa Damu ya Yesu, imo nguvu ndani ya hiyo Damu...

KWANINI TUNAFUNGA NA KUOMBA

  Kwa nini tunafunga? Ni sawa na tunamwambia Mungu kuwa tunataka kurejea kwako, tutembee na wewe na tuwe na wewe, kwa kusudi gani? Ili tupate KUSTAWI. NINI MAANA YA USTAWI? ·          Ni maisha ya kumeondokana na uhitaji yaani ni maisha ya utoshelevu, ·          Ustawi maana yake ni utimilifu wa mtu, pasipo ustawi bado haujatimia. ·          Ustawi maana yake umeufikia wito ambao Mungu amekuumbia, Mungu alimuumba mwanadamu kwa sura na mfano wake, kwa kusudi gani? Ili afanane naye. Katika Mungu hakuna labda labda bali kuna utimilifu. Biblia inasema nini kuhusu Ayubu? Ayubu alikuwa mtu mkamilifu, nini maana ya ukamilifu? Maana yake alikuwa ni mtu aliyestawi. Alikuwa na watoto, wanyama na watumwa walio mzunguka wa kiume na wakike, ustawi maana yeke ni utimilifu wa mtu . Ayubu 1:1 “Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo...