Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 7, 2023

UKOMBOZI NA UPONYAJI

 Ukombozi na Uponyaji. Paulo na sila walifungiwa mahali kwa sababu mapepo waliamua kumtumia mfalme ili kuliharibu kanisa, waliwafungia mahali wakifikiri kuwa sauti zao hazitasikiwa, lakini ilipofika usiku Paulo na Sila wakaamua kuimba na walipoimba Mbingu ilishangaa na kuja kuwasaidia. Kuna miujiza itatokea ambayo haujawahi kuiona, inaweza ikawa unataarifa mbaya kutoka kwa madaktari kuwa kutokana na ugonjwa ulionao inapaswa utolewe kizazi na hautaweza kuzaa tena, au umeambiwa ugonjwa ulionao hauna dawa, na wengine wameambiwa kuwa ugonjwa ulio nao utakuwa nao mpaka ufe, sikia nikwambie ni hivi ibilisi ndio atakayekufa na huo ugonjwa lakini si wewe, Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako. Unaweza ukawa katika ukoo wenu hakuna aliyewahi kuendesha gari na wewe na kaka zako na mabinamu zako hakuna anaye endesha gari kwa sababu mmefungiwa mahali, lakini leo utatoka kwa Jina la Yesu. Yesu hakwenda msalabani kwa ajili yake mwenyewe, bali alikwenda kwa ajili yako, siku ile Yesu alimshinda ib...

KUONGOZWA NA ROHO

 KUONGOZWA NA ROHO. Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:- 1.      Afanye kazi, 2.      Awe na umiliki juu ya nchi, 3.      Azalishe, 4.      Aombe, 5.      Ashuhudie, 6.      Aabudu, 7.      Lazima awe mtoaji, 8.      Lazima uwe na upendo, penda uumbaji, 9.      Lazima asamehe na atubu, 10.  Ahakikishe anatunza wito wake.   Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda,   1 Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” Mungu ametupa ufunuo kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini, maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo kuhusu wewe, Mungu au ya ibilisi yaliyo katika roho hiki ndicho tunakiita ufunuo inamaana yamefunuliwa kwako. Biblia inasema “Lakini Mu...