Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ELIMU YA JAMII

ASILI YA MWANA DAMU

Picha
  Wanasayansi nchini Canada na Marekani wamechapisha utafiti ambao unakosoa nadharia ya sasa kuhusu asili ya mwanadamu wa sasa kwamba ni katika Afrika. Wakiangalia katika data za urithi, watafiti kutoka Chuo kikuu cha McGill na Chuo kikuu cha California - Davis wanasema kulikuwa na watu wengi waliokuwa wanaishi katika sehemu nyingi za Afrika, wakihamia kutoka kanda moja kuelekea nyingine na kuchanganyikana kwa zaidi ya miaka maelfu kadhaa. Matokeo haya ya utafiti yanakinzana na nadharia kwamba binadamu wa sasa- Homo Sapiens ni kizazi cha mababu waliokuwa wakiishi Mashariki na Kusini mwa Afrika. “Katika vipindi tofauti, watu walikubaliana na nadharia kwamba asili ya Homo Sapien inaonyesha kuwa binadamu kwanza walitokea mashariki au Kusini mwa Afrika,” alisema Brenna Henn, mtaalamu wa urithi katika chuo kikuu cha California, Davis ambaye pia ni mwandishi mkuu mwenza wa utafiti. “Lakini imekuwa vigumu kukubaliana kuhusu nadharia hizi kutokana na uchache wa mabaki ya watu wa kale na re...

siri ya mafanikio ya mtu tajiri zaidi duni

Picha
  Ijue siri ya mafanikio ya mtu tajiri zaidi dunian CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Mwaka 2004, Jeff Bezos na mshauri wake wa masuala ya kiufundi Colin Bryar walisafiri pamoja hadi mji wa Tacoma, umbali wa saa moja kusini mwa jiji la Seattle jimbo la Washington. Wakati huo, thamani ya kampuni ya Amazon ilikuwa mabilioni ya dola. Hata hivyo, walikuwa wanaelekea katika kituo cha kuhudumia wateja cha kampuni hiyo - kwa siku mbili walifanya kazi kama watoa huduma kwa wateja. "Jeff alikuwa akipokea simu zinazopigwa na wateja yeye mwenyewe," Bryar anasema. Anakumbuka malalmiko ya moja ya bidhaa yalivyokuwa yakiendelea kuripotiwa kila wakati. "Jeff alishituka. Macho yalimtoka." Bezos alikuwa ametatizika. Bila shaka yoyote bidhaa hiyo ilikuwa na hitilafu, lakini suala hilo halikuripotiwa katika ngazi za juu. Baadaye siku hiyo hiyo, alituma ujumbe kwa njia ya barua pepe akitaka apewe mapendekezo ya namna gani ya kuripoti bidhaa zenye matatizo sokoni.Bezos anajiuzulu wadhifa w...