Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 22, 2023

UTOAJI

 *UTOAJI MBELE ZA MUNGU UNAVYOWEZA KUKUFUNGULIA MLANGO MKUBWA WA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO* *Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya*  (1 Wafalme 17:16) Siku ya leo tutafakari kwa kina ujumbe huu  *Kila kitu ni utoaji* na hakikisha unasoma na kuchukua hatua. 👉Yaani Kama hautoi basi pia hupokei. Na kama haupokei basi hutoi.  ✅Utoaji ni daraja kati ya mafanikio yako na wewe ulipo. Utoaji ni mbegu, ambayo baadaye itakuzalia matunda. ◾Jiulize wewe unatoa nini? ◾ Unatoa kwa nani?  ◾Unatoa wapi?  📌Watu waliofanikiwa tabia moja wapo inayofanya wafanikiwe ni utoaji. ✅ Kwa wale wasomaji wazuri wa biblia,  imebainisha bayana kabisa kuwa, heri kutoa kuliko kupokea.  ✅Kwa maana anayetoa atapokea na kuongezewa zaidi. ""Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya *Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwen...

NDOTO

Ndoto ni njia mojawapo ambayo Mungu husema,na kuwaelekeza watoto wake waleo. YOWELI 2:28-29 Shetani pia huzungumza,hushambulia na kuwamiliki watu kupitia ndoto.Maombi yenye nguvu yanaweza kukuwezesha kuyashinda mashsmbulizi kama hayo ya ndoto.Jifunze kushughulika na ndoto ili kupambana na ndoto za vitisho na za uongo za shetani. ZEKARIA 10:2 AINA ZA NDOTO. i)Ndoto za ki-binadamu. Hizi hutokana na shughuli nyingi tunazoshinda nazo za kila siku. MHUBIRI 5:3 ii)Ndoto za ki-pepo(shetan). Hizi ni ndoto za vitisho ,uwongo na mashambulizi juu ya wanadamu zisababishwazo na nguvu za giza ili kuwamiliki na kuwatawala wanadamu. YUDA 1:8 iii)Ndoto za Ki-Mungu. Hizi ni ndoto zitokanazo na Mungu ili kutupasha taarifa Fulani katika maisha yetu.Mungu hutupa maelekezo mbalimbali kwa njia ya ndoto ili tuweze kumshinda mwovu. HESABU 12:6 YEREMIA 23:28 KITABU CHA AYUBU 33:13-17 Ifuatayo ni mifano ya watu waliopewa maelekezo na Mungu kwa njia ya ndoto kibiblia. i)ABIMELEKI Mungu alimkemea Abimeleki mfalme ...

AINA ZA MAOMBI

 *AINA ZA MAOMBI.* *1. MAOMBI YA KUWAOMBEA WATU WENGINE (MAOMBEZI).* -Kwa mtu aliyeokoka ni lazima uwaombee watu wengine, mojawapo na sababu inayomfanya Mungu ajibu maombi yako lazima usiwe mbinafsi jali na wengine kwa kuwaombea. -1 SAMWEL 12:23 Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka -EZEKIEL 22:30 Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. 31 Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU. FAIDA YA MAOMBI YA KUWAOMBEA WATU WENGINE (MAOMBEZI). -Yanaimarisha kanisa katika misingi ya Umoja na Upendo.  -Inajenga nafasi nzuri ya Mungu kuanza kutenda kwako. -Yanawajenga watu wengine waweze kusimama vizuri kwenye wokovu (mfano maombi ya washirika juu ya viongoz...