Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 28, 2021

Kwa Wewe ambaye bado hujaolewa,

  Kwa Wewe ambaye bado hujaolewa, usitafute kuolewa na Malaika (mwanaume asiye na mapungufu) hutakaa umuone hata mmoja, mimi nawafahamu wanaume, mwanangu hutakaa umpate asiye na udhaifu (mapungufu) lakini kabla hujaolewa angalia hicho kichwa kinachokuoa kikoje? Angalia AKILI yake na usiangalie leo ana nini, inawezekana hana pesa nyingi leo lakini kama ana AKILI pesa zitakuja.   Elewa yule anayekuoa ana udhaifu na Mungu anakupeleka kwake ili ukaushughulikie. Hakuna udhaifu usioleta aibu bali ukiuona udhibiti. Mwingine udhaifu wake ni hasira anapiga watu au hata wewe anakupiga, ukiona hivyo usibebe vitu ukakimbia bali kumbuka umepelekwa pale ili kudhibiti huo udhaifu.   Mwanaume yeyote anayempiga mke wake ni mpumbavu na ili kuondoa huo upumbavu wewe kama mke jifunze kumsifia, mwambie namshukuru Mungu kwa kunipa mume kama wewe, sifa zinaondoa ujinga.   Mwambie Mungu akutie Nguvu ili upate kushinda na sio kukimbilia kudai taraka kwa maana Mungu anachukia kuachana .

MATUMIZI YAKO

  Jitahidi matumizi yako yalingane na mapato yako wala yasivuke kiwango kinachotakiwa vinginevyo utakuwa na madeni au utaiba na mwivi ni mzigo kwa wengine. Angalia matumizi yako yasiingilie akiba yako ukashindwa kufika ulikokusudiwa. Usiige maisha ya watu wengine au kujiweka daraja la juu kwa kuombaomba, huo ni upumbavu, bali ishi katika daraja lako. Jipime unatumiaje muda, fursa, nguvu na mapato yako. Kwa nini uishi nyumba usiyomudu wakati uwezo wako ni mdogo? Ishi kwenye nyumba yako hata kama siyo ya bati maana Mungu anatukuzwa kwa kilicho chako. Waamini wana tatizo la kupenda vitu vya bure, ni kosa kubwa kupanga nyumba ya mtu bila kulipa. Wokovu ni bure, lakini siyo rahisi, una gharama na Yesu alikufa kwa ajili hiyo. Mtakatifu kama hana fedha, anaweza kusahau kama ameokoka; kwa hiyo pambanua mambo ya siku zote na yale maalumu ili ujue kipi cha kufanya kwanza. Walawi 10: 8-10 "Kisha BWANA akanena na Haruni, na kumwambia, usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoj...