Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HABARI ZA UCHUMI

chanzo cha moto Kariakoo Kuchunguzwa

Picha
    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atembelea soko la Kariakoo kushuhudia hasara iliyosababishwa na moto. Picha kwa hisani ya Global Publishers TV, Dar es Salaam, Tanzania. Kufuatia kuungua moto Soko la kimatiafa la Kariakoo Jijini Dar es salaam, nchini Tanzania, Serikali imeunda tume kuchunguza chanzo cha moto huo ulioteketeza maduka zaidi ya mia nne yalioko katika jengo la Soko hilo maarufu. Viongozi mbalimbali wametembelea eneo hilo wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambaye ameagiza uchunguzi huo kufanyika ndani ya siku saba. Pia Majaliwa ameahidi kuwa serikali itazungumza na mabenki yaliyo wakopesha Wafanyabiashara waliounguliwa na maduka yao. Aidha changamoto ya vifaa kwa Idara ya Zimamoto pamoja na miundombunu hafifu katika eneo hilo vinaelezwa kuchangia pakubwa athari zaidi za moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa moja jioni Jumamosi tarehe 10 na kuteketeza maduka na mali za wafanyabiashara katika soko hilo. Tathmini halisi ya hasara iliyosababisha na ...

Soko Kuu Mombasa lateketea kwa moto

Picha
  Soko maarufu la Marikiti mjini Mombasa nchini Kenya limepata hasara kubwa kutokana na moto ambao ulilikumba soko hilo Jumamosi usiku kuamkia Jumapili. Wafanya biashara katika soko maarufu la Marikiti mjini Mombasa wamepata hasara kubwa baada ya moto mkubwa kushuhudiwa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Hakuna ripoti za maafa wala majeruhi kufikia sasa huku juhudi za kuzima moto huo zikiendelea. Magari ya zima moto kutoka kitengo cha serikali za ugatuzi wakishirikiana na polisi wako kwenye tukio wakijaribu kudhibiti hali. Wakati huu ambapo kuna sharti la kutotoka nje wakati wa usiku kwa sababu ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, baadhi ya wakaazi wa maeneo ya karibu wako nje kushuhudia moto huo na wengine wakitoa msaada wa kudhibiti moto. Hali hii imewalazimu maafisa wa kushika doria nyakati hizo kuweka usalama eneo hilo pia kuepusha visa vya uporaji kutokea kwenye baadhi ya maduka yaliyoachwa wazi kutokana na moto huo. Haijabainika chanzo cha moto huo, na hakuna mwenye kuf...