Italia 3-2 kupitia penalti
Italia 3-2 kupitia penalti CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Matumaini ya kumaliza ukame wa miaka 55 bila taji kubwa yalivunjwa jana kwa kushindwa na Italia kupitia mikwaju ya Penalti na kuipa Italia ushindi wa kombe la Euro 2020 uwanjani Wembley Italy, ambao hawajashindwa katika mechi 33 kabla ya fainali walijirejesh polepole mchezoni na wakasawazisha katika dakika ya 67 baada ya England kutangulia kufung mapema katika kipindi cha kwanza . Baada ya kipindi kigumu cha muda wa ziada ,mshindi hakupatikana timu hzo zilipotoka sare ya bao moja na ikalazimu mikwaju ya penalti kutumiwa kumpata mshindi .Huo ndio uliokuwa mwanzo wa mafadhaiko ya kocha Gareth Southgate na wachezaji wake walioingia fainali kwa matumaini makubwa . England ilikosa kufunga mikwaju mitatu ya penalti kati ya mitano waliopewa huku wachezaji Marcus Rashford ,Jadon Sancho na Bukayo Saka wakikosa kufunga Harry Kane na Harry Maguire waliifungia England ilhali Pickford mikwaju ya Andrea Belotti na Jorginho ilhali Domeni...