NGUVU YA DAMU YA YESU
NGUVU YA DAMU:
Damu ya Yesu ndiyo inayomfanya mwamini awe mtakatifu wa Mungu,
hauwi mtakatifu pasipo Damu ya Yesu kukusafisha. Unahitaji damu ya Yesu
kukusafisha ili uwe mtakatifu wa Mungu. Haki huja kupitia Neno lakini utakatifu
huja kwa kupitia damu. Katika damu ndipo ukombozi ulipo, huwezi kutoka
kwenye dhambi na uovu ambao unaokufanya usiwe mtakatifu pasipo Damu ya Yesu, ni
kwa Damu pekee ndiyo itakufanya uwe mtakatifu wa Mungu na huo utakatifu ndio
unamfanya Mungu avutiwe na wewe. Utakatifu wako ndio utakao mvutia Mungu lakini
ili uupate ni lazima uipate Damu ya Yesu na hapo ndipo ukombozi ulipo. Nguvu
inayo fukuza dhambi zote maradhi na magonjwa ni damu ya Yesu, kupitia Damu
tunao ukombozi wetu, wokovu, utakatifu, tunakuwa washiriki wa mambo ya
mbinguni.
Ufunuo 12:11 “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao;
ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”
tunamshinda adui, maradhi na magonjwa kwa Damu ya Yesu, imo nguvu ndani ya hiyo
Damu. Katika maisha yako Damu ya Yesu ni ya muhimu sana ili uwe na ushindi na
kupitia hii ndipo mwamini atashinda kila aina ya changamoto humu duniani.
Isaya 53:5 “Bali
alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu
ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” kuchubuliwa kwake kulisababisha damu imtoke kwa ajili yetu,
kwa kupitia damu yake tunakuwa washiriki wa uzima.
UPAKO:
·
Upako huvunja nira,
·
Unakuondoa kunako mizimu,
·
unakukutoa kutoka katika
ya kale.
·
Upako unakutoa kwenye
mambo yanayo kushikiria na kuvuta nyuma.
Isaya 10:27 “Tena
itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake
shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.” Kama kuna nira zinazo kufuatilia iwe ni za kifamilia unahitaji
upako ili kuzivunja hizo nira.
Mafuta ya upako ni nini? Ni tunda la mzaituni ambalo kwa
nyakazi za kale walikuwa wanatumia kwa matumizi yafuatayo:-
·
Yalitumika kuwasha taa
hekaluni,
·
Yalitumika kama mafuta
yakujipaka mwilini,
·
Yalitumika kwa ajili ya
kupikia,
·
Yalitumiwa kuweka wakfu
kitu kitakatifu kama nyumba au vyombo vitakavyotumika hekaluni.
·
Yalikuwa ni kwa ajili ya
kusimikwa kwa watumishi wa Mungu aliye juu; lengo la kuwapaka mafuta hayo ni
kuonesha kwamba mtu huyu yupo chini ya wito wa Mungu na kwa kufanya hivyo roho
wa Mungu mwenye enzi yote alikuja juu ya huyo mtu ili kumuwezesha kwa ajili ya
kazi takatifu za Mungu. Tunaweza kuona Musa alipofanya hivyo kwa Haruni na
Samweli kwa Daudi; jambo hilo Yesu alifanya kwako wewe ambaye umeokoka, baada
ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako roho yule yule aliyeishi
kwa Yesu yumo ndani yako.
Kupitia huo upako unayo nguvu ya kufukuza mapepo, unayo nguvu ya
kuponya wagonjwa na kufukuza maradhi. Kwa huo upako tunayo nguvu ya kuziharibu
kazi zote za ibilisi.
Ombi:
Simama katika zamu yako
na mfukuze ibilisi katika chochote alicho kuibia au kukiharibu katika maisha
yako.
Maoni