JINSI YA KUMFANYA MUNGU AFURAHI.

 

JINSI YA KUMFANYA MUNGU AFURAHI.

 Biblia inasema Roho wa Bwana anatusaidia kumfanya Mungu afurahi. Pia anatusaidia kuomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu, wakati mwingine tunafikiri kuwa tunajua kuomba na kumfanya Mungu asikie lakini tunapiga kelele tu. Tunaweza kufunga na kuomba kwa kitambo lakini Mungu hawezi kusikia kwa sababu wakati mwingine anasikia kelele.

Tufanyaje ili kumsababisha Mungu asikie? Tunamfanya Mungu asikie pale tunapo omba sawa sawa na mapenzi yake.

 

1 Yohana 5:13-14 “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”

Ukiomba sawa sawa na mapenzi ya Mungu YEYE anatusikia; kuna mapenzi kwa ajili ya mwaka huu, kwa ajili ya mwaka jana na kuna mapenzi kwa mwaka ujao na yako pia mapenzi ya Mungu kwa ajili yako. Yako mapenzi kwa ajili ya Tanzania sasa yapasa kuelewa, kwamba unataka kuomba sawa sawa na mapenzi ya hii nchi utapata kwa sababu Mungu anamipango nayo lakini ukiomba tofauti hautaweza kupata.

 

Roho wa Bwana anatusaidia kujua mapenzi yake na siyo hicho tu bali pia anatufanya sisi tuombe sawa sawa ili tuweze kupata kile tunacho kiomba.

Yohana 8:13 “Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli.” Unapo fanya jambo kwa niaba yako unaweza kukosa, lakini Roho akichukua nafasi kwa niaba yako anajua unahitaji nini na Mungu anahitaji kitu gani kwako, hivyo anawaungamanisha pamoja.

Yohana 16:8 “Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” Akija huyo Roho wa kweli atakuongoza kwa ajili ya mambo matatu:

1.      Dhambi,

2.      Haki na

3.      Hukumu.

Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” Roho anapokuja kwako atakuja akiwa na wajibu kutoka kwa Mungu kwa ajili yako, anapo kuja kwako anakuja na kazi ya pekee.

Anapo kuja huyo Roho wa Kweli kwako, atakuongoza sawa sawa na kile ambacho Mungu ameweka kwako, atakueleza dhambi ni nini, ibilisi ni nani na uzima wa milele ukoje. Yeye atakuongoza na kukupeleka katika kweli yote kuhusu wewe na kuhusu Mungu na maisha yako katika kweli yote.

Wakristo wanapaswa kufahamu mambo haya manne:-

1.       Mambo ya siku zote yaani mambo ya kawaida, kula kufanya kazi kwenda huku na kule.

2.       Mambo najisi, kwa sababu Mwamini sio mtenda dhambi lakini anaweza kujinajisi au kunajisika. Mfano wakristo waliozaliwa mara ya pili wanatalikiana wanajinajisi wenyewe.

3.      Mambo yaliyo safi; kumsaidia mwingine, kumfurahisha rafiki yako ni jambo safi lakini halitokani na Mungu, Unaweza fikiri upo na Mungu lakini haupo nae bali upo na dunia.

4.      Mambo Matakatifu; Hili ndilo tendo la Roho na hiki ndicho kitakufanya uwe MKUU na kuingia Mbinguni.

Matendo 10:1-3 “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!……”Ndio Mungu ameona tendo lako, lakini haujakubalika uingie Mbinguni. Ni kitu gani kinacho kusababisha wewe uingie mbinguni? Ni Utakatifu na kumruhusu Roho wa Mungu akuongoze.

Yapasa kufahamu pasipo Roho kutuongoza kutoka ndani hatuwezi kumpendeza Mungu. Tendo la Imani ni MAONGOZI YA ROHO MTAKATIFU KUTOKA NDANI.

 

Roho alikuja siku ya Pentekoste na mpaka leo bado yupo huku duniani ili amuwezeshe mtu mmoja kuingia ndani yake na apate kumuongoza katika mapenzi ya Mungu.

Siku ulipo mpokea Yesu, Roho ya Kristo ilikujilia ndani yako, hii ndiyo tunaiita ulizaliwa mara ya pili. Baada ya wewe kumkubali Yesu kuingia ndani yako na akakufanya uwe mtoto wa Mungu, hii ndiyo kazi yake.

 

Anapokuja anakufanya mtoto wa Mungu, sasa unahitaji kukubaliana na hilo ili upate kukua pamoja naye. Unafanyaje? Anapo kuja utajua kuwa yupo ndani yako pale unapo anza kunena kwa lugha mpya. Unapo anza kunena kwa lugha, Roho wa Mungu anaisukuma ile Roho ya Kristo ipate kulia kama vile mtoto anavyolia kwa ajili ya kuponya ili kupata msaada kutoka kwa Mungu.

Kunena kwa lugha kunakusaidia kujijenga mwenyewe, kumjenga yule mtu wako wa ndani. Kunena kwa lugha kuna kusaidia kujisafisha kutoka ndani kuja nje. Hivi ndivyo tunavyo jisafisha na kujijenga wenyewe. Maana yake tunakuwa Hodari Kiimani, katika Neno, Kiroho, Kimaombi, katika Udhihirisho wa Roho Matakatifu, kufanya Uponyaji na Ukombozi na Miujiza. Roho wa Mungu ndani yako ni wa muhimu mno.

 

1 Wakorintho 14:39 “Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha.” Kwa nini kuhutubu? Kwa sababu unapoenda kushuhudia na kuhubiri unaleta mtu mmoja kwa Kristo hivyo unakuwa unawaleta wengine kwa Kristo lakini unapofanya hivyo usizuie kunena kwa lugha mpya kwa sababu kunena kwa lugha mpya kunakusaidia wewe na sio mwingine.

Tambua kuwa Roho wa Mungu ndani yako ana nguvu ya kuhuisha mwili wako ulio katika hali ya kufa. Warumi 8:11 “Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.”

Roho akaaye ndani yetu huhuisha miili yetu.

 

Maoni