Nguvu ya Mwamini.
Nguvu ya Mwamini.
2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya
Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.” Hauhitaji kukumbuka ya jana kwa maana yamekwisha, ni kwa
nini haupokei kutoka Mungu? ni kwa sababu wewe unawaza ya jana.
Mungu hana mpango wa jana yako, kwa nini? Kwa
sababu jana ni ya kale na imepita, Mungu anampango na nini? Mungu anampango na
leo na kesho yako, Mungu ana shauku mno na kesho yako, kama unataka kutembea na
Yeye zingatia mapenzi yake, mapenzi yake sio jana yako bali mapenzi yake yapo katika
kesho yako.
Kama upo ndani ya Kristo na umezaliwa mara ya
pili yaani umeokoka Mungu anashauku sana na wewe, anasema jana yako imepita.
Jana ni mambo ya kale, je ni nani anaye zingatia mambo ya kale? Tunatumia vitu
vya kale kwa ajili ya kuvitazama tu tunaenda katika makumbusho ili kuona vitu
vya zamani tu, hauzingatii sana vitu vya kale. Kwa nini unampango sana na jana
yako wakati jana yako imepita, ilihali hata nguo zako za jana umeziweka pembeni
na nguo mpya unaziweka mahali pazuri.
Mungu akakukumbuke leo hata kama haujawahi
kupata kitu kipya akakupe.
Chochote kilicho kipya kina nguvu; Unakuwaje mpya?
1 Yohana 4:4 “Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu
nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye
katika dunia.” Chochote kipya hukishinda cha kale katika bei, kung’aa,
nguvu, kukaribisha, kuvutia. Kipya ni zaidi ya cha zamani, ibilisi alikuwa
akikusumbua ni kwa sababu ya jana, kama magonjwa yalikuwa yanakusumbua ni kwa
sababu ya jana, kama ulikuwa katika njaa ni kwa sababu ya jana yaani yakale,
kama ulikuwa umekataliwa ni kwa sababu ya jana, ya kale mara zote hukataliwa
wala hayavutii.
Kama wewe una maradhi ni kwa sababu ya jana,
ukikutana na kitu kilichokufa utakutana na wadudu, nzi n.k, ulikuwa unafatwa na
magonjwa n.k ni kwa sababu ya jana.
Kalebu akasema “sasa nina miaka 65 lakini
nina nguvu za kivita kama nina miaka 40” kwa nini Kalebu alisema hivyo? Kwa
sababu ya kale yalikuwa yamepita na Mungu akampeleka katika mapya akawa kama
ana miaka 40. Je wewe unajisikiaje? Wewe ni mtoto wa Mungu ni kwa nini
unapigana na mambo? Ni kwa sababu umebeba ya jana.
Mimi nilikuwa ninasumbuliwa na magonjwa,
umasikini n.k kwa sababu nilikuwa nimebeba jina la babu wa babu na babu wa babu
hivyo nikawa nimebeba ya jana, lakini sasa baada ya kuokoka nikafanyika kuwa
kiumbe kipya yakale yakapita na nikawa kiumbe kipya, sisumbuliwi na magonjwa,
chakula sio shida kwangu. Ukiokoka unafanyika kiumbe kipya ya kale yanapita
kamwe hautasumbuliwa na chochote.
Zaburi 91:1-2 “Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli
wake Mwenyezi. Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu
wangu nitakayemtumaini.”10-11 “Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema
yako. Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.”
Ukiwa mtoto wa Mungu unajificha chini ya uvuli wake
hakuna mabaya yatakupata, wewe ni kiumbe kipya.
Kumbu kumbu 5:1-3 “Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi
Israeli, zisikieni amri na hukumu ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza
na kuangalia kuzitenda. Bwana, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika
Horebu. Bwana hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi
sote tuliopo hapa, tu hai.” Kama umezaliwa mara ya pili (umeokoka) lazima uangalie
katika kutenda sawa sawa na ulicho fundishwa na sio mafundisho ya zamani uliyo
jifunza kwa baba zako au dini yako.
Unapokuwa kiumbe kipya utatenda haya: Marko 16:18 “watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha
kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao
watapata afya.”
Ukishafikia kuwa mpya hakuna kitakachokudhuru huku
duniani iwe ni ugonjwa, uchawi, mapepo, au chochote kinacho sumbua uhai wako
hakina ruhusa.
Mambo yanayo mpa mwamini nguvu apate kushinda ya kale.
1. Toha, 1 Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu
na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” toba inakuletea usafi
kwa sababu ya kale mara zote hunuka vibaya, chochote cha zamani kinatoa harufu
mbaya. Unapo tubu usafi huja ili usafishwe na ndio maana toba ina nguvu, usafi
unapo kuja yakale hayana nguvu tena, mambo ya kale yanayotesa sana ni mapepo,
maradhi magonjwa, sasa unapo tubu vinakuwa havina nguvu maana unakuwa
umesafishwa.
Zaburi 103:3-4 “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako
yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,”
·
Anakusamehe maovu yako kwa sababu umetubu
·
Anakuponya magonjwa yako yote
·
Anakomboa uhai wako na kaburi na kisha anakutia taji ya
fadhili na anakupa Rehema zake.
Kuna nguvu katika toba na ibilisi anajua
Mathayo 9:1-6 “Akapanda chomboni, akavuka, akafika mjini
kwao. Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye
Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu,
mwanangu, umesamehewa dhambi zako……..”
·
Hapa unaweza kuona nguvu ya toba, toba inaleta uponyaji
na ukombozi
·
Maombi yako yanasikiwa pale unapo tubu
·
Huachilia Damu ya Yesu ije kwako kwa ajili ya kukusafisha
na kukukomboa.
Isaya 59:1-2 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa
wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu
yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake
msiuone, hata hataki kusikia.” hapa inamaana kuwa dhambi inakuzuia ili
usisikiwe hivyo kupitia toba mlango unafunguliwa ili upate kusikiwa.
Kama unataka kuyashinda ya kale na uwe mpya ni lazima
utubu.
2. Maombi: maombi
yatakufanyaje kuwa mshindi? 1Yohana 5:18 “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu
hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu
hamgusi.” Unapo jua kile kitu ambacho Mungu anafanya kwako ndipo
unapaswa kuomba, usiombe kabla haujatubu
·
1Yohana 5:14 “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba
kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.” Tutajuaje mapenzo ya Mungu? Ni mapenzi ya
Mungu kukuona wewe ukitubu, hivyo unapo tubu unasababisha maombi yako yasikiwe.
·
Usiombe bila kufahamu Neno bali fahamu kwanza ndipo uombe
ili ujue nini unahitaji kuomba, Isaya 65:24 “Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba,
nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Hii inamaana kuwa kuna watu wa aina fulani
wamekaribishwa mbele za Mungu ili wapate kuona na si kila mtu.
·
Toba inakufanya wewe uwe safi, baada ya wewe kutubu
unakuwa safi na Mungu akitazama moyo wako anaona nia yako lakini kama haujatubu
Mungu anaona dhambi yako na siyo nia yako hivyo hawezi kujibu maombi yako.
·
Mahali ambapo uwepo wa Mungu upo hakuna madhara, Isaya
65:25 “Mbwa-mwitu
na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na
mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima
wangu mtakatifu wote, asema Bwana.” hii inamaana kuwa kama umezaliwa mara ya
pili Mungu anaishi ndani yako uwepo wake utakufunika kila mahali, popote
utakapokwenda sumu haita kudhuru, wakati wengine wanakufa na magonjwa wewe
unaudhihaki huo ugonjwa, wakati wengine wanatishika mno wewe unacheza kwa
furaha.
Isaya 65:25 “Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba
atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru
wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana.” Ukiwa katika mlima wa
Bwana hauhofii chochote, hakuna madhara wala mpambano ambao unaweza kukushinda.
Wewe panda kunako huo mlima wa Bwana ishi hapo, sema
kutoka hapo, tembea kutoka hapo, furahi, cheza, omba ukiwa hapo utakuwa salama.
Katika mlima wa Bwana ni mahali gani hapo? Ni hapo ambapo mtumishi wa
Bwana alipo.
Mlima wa Mungu sipo alipo bali ni mahali ambapo waabuduo
walipo, popote utakapokwenda unakuwa mlimani mwa Mungu, sasa nini kitatokea?
Roho wa Mungu atakuwa na wewe wakati wote ili kusababisha mlima wa Mungu
kuwepo.
Kwa nini maombi? Luka 3:21-22 “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na
Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; Roho Mtakatifu
akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni,
Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.”Umuhimu wa wewe kuomba ni
huu:-
·
Inakusaidia kufungua mbingu na utamfanya Mungu aweke tangazo
la kukutambulisha kwa ulimwengu.
Unapoomba unamfanya Mungu awe makini kwa ajili yako.
Hakikisha unafanya maombi ili kumfanya Mungu amakinike na wewe.
·
Zaburi 34:4-7 “Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu
zote.Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona
haya. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia, Akamwokoa na taabu zake
zote. Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.” Kupitia maombi ukombozi
unatokea kutoka kwenye hofu, kwa sababu hofu ni ugonjwa hatari sana.
·
Mtu anaye fanya maombi mara zote anapendezwa na maswala
ya kiroho.
·
Nyuso za wana maombi hazitatiwa aibu, kamwe hautaweza
kuona uso wa mwana maombi akiwa na aibu haijalishi atapitia hali gani.
·
Watu wanao omba wanaokolewa na masumbufu, malaika huweka
kituo akiwazungukia
3. 1 Nyakati 4:9-10 “Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko
nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa
kwa huzuni.Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba
ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa
pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu
akamjalia hayo aliyoyaomba.” Ukiomba kama Yabesi alivyo fanya nini kinatokea,
·
Maombi ni chombo cha kubadilisha hali yako, ukiwa katika
hali fulani tamani kuomba ili maombi hayo yakabadilishe hiyo hali.
·
Maombi ni ufunguo wa kutafuta msaada toka mbinguni pale
ambapo chanzo cha kuzaliwa kwako upya kilipo toka.
·
Maombi huchukua aliye dhaifu awe na nguvu na ujasiri
mbele za mpinzani wake, unaweza ukawa dhaifu kiuchumi lakini kupitia maombi
ukajitia nguvu uchumi wako ukabadilika na ukajitia nguvu katika hiyo hali yako.
Mwamini ana vyanzo vingi vya nguvu, chanzo cha nguvu
inayotokana na neno.
·
Yeremia 23:29 “Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo
ivunjayo mawe vipande vipande?” wakati mwingine waweza ukajihisi kama upo
jela au uko mahali kama kichakani hauoni hata msaada, hivyo utatumia Neno la
Mungu kama nyundo ili kuvunja hilo gereza.
·
Zaburi 119:105 “Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.” wakati mwingine waweza
ukawa unatamani kutimiza jambo fulani lakini hauwezi hivyo Neno linakuwa
ni nuru yako ili uweze kuona njia ya kutoka au kuingia.
Neno ni kwa ajili ya wale wanaotaka kuona mpenyo, watu
wanaotaka kusonga mbele wanahitaji Neno.
·
Yohana 6:52-59 “Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje
mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?Basi Yesu akawaambia, Amin, amin,
nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna
uzima ndani yenu……. .” Watu wanajiona wao ni dhaifu ki mwili, katika maisha
wanahitaji Neno liwe kama chakula kwao.
·
Waebrania 4:12 “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina
ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya
nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi
kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” Neno linakusaidia kufukuza hofu na mashaka
kwa sababu kama ukiwa hauna hofu na mashaka utatamka jambo nalo litatokea.
·
Isaya 55:10-13 “Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka
mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na
kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;…..” ukilila neno wewe
unakuwa Neno, hivyo ukiongea unalisema Neno.
Ayubu 22:28 “Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga
utaziangazia njia zako.” Hakuna atakayekuangazia bali wewe
Zaburi 107:20 “Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika
maangamizo yao.”
Maoni