MIAMBA YA SOKA TZ sasa Yasubiriana Kigoma

 

MIAMBA YA SOKA TZ sasa Yasubiriana Kigoma

JULai 06 2021
full pic

BAADA ya Yanga juzi kuilaza Simba bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, mashabiki wa timu hizo jijini hapa wamesema watakutana Julai 25 huko Kigoma na mbabe atajulikana zaidi msimu huu.

Katika mchezo wa juzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga iliichapa Simba na kufikisha pointi 70, ikiachwa alama tatu na wapinzani hao, huku ikiwa mbele kwa mechi mbili.

Simba waliingia uwanjani wakihitaji ushindi ili kutangazwa mabingwa lakini Yanga walikuwa makini kuharibu mipango na kufanikiwa kupata bao mapema kupitia Zawadi Mauya na kufanya ligi kuendelea kuchangamka upande wa ubingwa.

Baada ya mchezo huo wa ligi, timu hizo zinatarajia kukutana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) utakaopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Sebastian Mwandala ambaye ni shabiki wa Yanga alisema timu yao haiwezi kufungwa na Simba na kwamba hizo ni salamu kuelekea mechi yao shirikisho kuhakikisha wanamtesa zaidi Mnyama msimu huu huku akitamba kuwa watabeba kila kitu.

“Tulisema mapema, hata kabla ya mechi hii kuchezwa, hii Simba haiwezi kutufunga na hizi ni salamu kabla ya kukutana nao tena huko Kigoma, msimu huu lazima watuheshimu,” alisema Mwandala.

Naye Catherine Ipopo shabiki wa Simba, alisema mechi hiyo wapinzani waliwazidi na lazima wakubali matokeo, huku akiwaomba mashabiki kutokata tamaa bali kujipanga upya na mechi ya shirikisho.

“Mechi ya watani lazima mambo mengi yawepo, kiujumla wapinzani wetu walikuwa bora, hatuwezi kukata tamaa bali kujipanga kulipa kisasi mechi ijayo kwa sababu lazima tukutane tena Kigoma,” alisema Catherine.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU