POMBE NI ANGAMIZO LA UCHUMI TANZANIA






habari mpendwa msomaji wangu,

leo nimeona nitoe uelewa wangu huu ili niwashirikishe jamii ya kitanzania, hasa wapenda maendeleo na wale wanao tamani kuiona Tanzania ikikua kiuchumi, kutoka hapa tulipo, yaani uchumi wa kati wa chini, Nakwenda uchumi wakati wa kati hadi juu. 

suala la kodi ni suala mtambuka sana, wengi wa wafanya biashara walipa kodi huwaona wadai kodi kama adui zao na warudishaji wa biashara zao nyuma, hii ni kutokana na aina au namna ya wakusanya kodi wanavyo wachukulia walipa kodi na namna wanavyo wafikia kudai kodi, kodi ni mhimu sana ili nchi iweze kufanya miundo mbinu itakayo rahisisha wafanya biashara hao hao kukuza na kuongeza mzunguko wa fedha katika biashara zao, pia kodi inawezesha kila mwananchi kupata mahitaji mhimu ya kila siku hii ni kwa watu wote wafanya biashara, wafanya kazi, wakulima n.k.

sasa sitaki twende sana huko, acha tuone bajeti iliyo pita 2021-2022 

leo naegemea katika kipengele kimoja cha kushusha kodi katika vileo na kupandisha katika mafuta. jambo hili nimekua nikilitafakari sana hata sija lielewa taifa hili kwanini linajikabidhi kwa ibilisi wazi wazi. haija niingia akilini mwangu hata kidogo na bado natafakari niwapi hawa wapanga bajeti wanalipeleka taifa. kileo chochote  kinayo kazi ya kupunguza kati ya mambo yafuatayo,

1. ufanisi wa akili

2. ufanisi wa utu

3. ufanisi wa uelewa

4.ufanisi wa maamuzi

sasa naomba serikali itoe ufafanuzi wa haya mambo manne, je tunenda kujenga taifa la namna gani hapo baadae?. acha ni yafafanue haya mambo manne

1. ufanisi wa akili...... pombe siku zote inashusha uwezo wa akili kufanya kazi katika mambo yote, huleta kuto chukulia jambo kwa uzito na kufikiri vitu virahisi rahisi tu. yaani kama ni kiongozi mlevi atataka kupata kipato kwa njia za panya na haoni madhara yanayo weza kumpata hapo baadae, wengi wa viongozi hawa wameishia kusitishiwa vibarua vyao (kutumbuliwa) walevi wote hata familia zao hawazitunzi ipasavyo tunazo familia nyingi mtaani mwetu za walevi na tunaona maisha wanayo ishi na familia zao.

2. ufanisi wa utu,........ mlevi kiongozi haoni uchungu na mwanadamu mwenzie isipo kua mlevi mwenzie tu, kiongozi mlevi huzurumu wananchi wake haki yao na kuitumia kwa anasa hiyo haki ya wananchi wake, hana huruma na mtoto wa jirani wala hata wa nyumbani mwake pia, mtu huyu amesha athirika ubongo wake kwa kileo. ndio maana utawaona wananchi wakienda kuomba msaada kwa watu wanamna hii na utaona wakizungushwa zungushwa tu au hata kuambiwa sina chakuwasaidia, baadae utamkuta baa amehonga walevi wenzake na makahaba pombe za laki na kwendelea, hapo ndipo tunaona huyu mtu hana utu yaani ufanisi wa utu umeshuka hayupo kuwatumikia wananchi bali kujitumikia mwenyewe.

3.  ufanisi wa uelewa,....... mtu mlevi ni mzito sana kuelewa ndio maana walevi wengi wengi huwa hawakubali kupokea maamuzi mapya katika akili zao, siku zote huona kanakwamba wana onewa yanapo tokea mabadiliko yoyote hasa ya kiutawala, wao huendelea kuwa kama walivyo zowea na hii huwaletea matatizo sana katika utumishi wao, kiongozi wao anapo leta mabadiliko fulani hasa ya kiutawala wao huendelea na mazowea yao na mwisho wake huondolewa katika nyazifa zao kwa aibu, lakini tambua kwamba mlevi hata apate aibu gani yeye huona ni kawaida tu maana haelewi kama hiyo ni aibu, wapo viongozi fulani waliondolewa madarakani kwa aibu na kesho yake wakasikika wanatamba maeneo fulani eti wakijitetea.

4. ufanisi wa maamuzi,......... hakuna mlevi anaye weza kutoa maamuzi yaliyo sahihi, ndio maana sheria nyingi humchunguza mtu anapofanya tukio fulani la ajabu kama alikua amelewa au alikua mzima au nikichaa au mzima, walevi siku zote hawaleti mtazamo mzuri kwa jamii, wanayo maamuzi ya kishetani, ukiongozwa na kiongozi mlevi mara zote ataleta maamuzi yasio na mtazamo wa mbele, marazote mlevi huona kilichopo na si kijacho, huu ni mtazamo wa ibilisi, ibilisi huona ya leo tu na kuyashughulikia leo lakini madhara yake huja mbeleni. ndio maana leo hii tunaona madhara ya kuwa na viongozi walevi hapo awali wasio mcha Mungu waliliingiz taifa katika mikono ya ibilisi hata leo watumishi wa Mungu wengi wanahangaika kulinasua taifa hili mikononi mwa ibilisi, je kwa maamuzi haya katika bajeti hii nikipi kinaenda kutokea katika jamii?...............

mimi binafsi naiona Tanzania ya walevi ikija kwa kasi, siku zote walevi huwatetea walevi wenzao naina bei ya vileo ikipungua na kuongeza idadi ya walevi na pia ongezeko la wagonjwa wa magonjwa yatokanayo na kula vyakula vyenye vileo vikali,

binafsi naona walevi wakilala mitaroni na wabakaji wakiongezeka, pia naona kiwango cha mambukizi ya ukimwi yakiongezeka kwa kasi sana, lakini hapa sishangai siku zote mlevi hana huruma, yupo tayari kumuuza mtu mwenzie ili apate cha kununulia kileo, hapa kuna biashara ya vidonge vya ARV. inawezekana kuna mlevi mmoja anapata asilimia fulani kwa watengeneza ARV kama ilivyo kwa chanjo za covid 19. 

katika tawala zilizo pita tuliona kuweka tumaini kwa Mungu kwa kila jambo na iliwasaidia Watanzania kuepukana na mapigo mengi ya ibilisi.  mfano ajali zilipungua lakini sasa zinaongezeka tena za ajabu sana kwakua kuruhusu pombe ishuke bei ni kumfanya shetani apatikane kirahisi hivyo tutashuhudia uovu wa ajabu sana maana nikama tunaishi na shetani majumbani mwetu, tunashuhudia sasa watu wanabaka watoto wao wa kuwazaa wengine wanaua wake, watoto na hata wazazi wao, matukio kama haya yalikua ni adimu sana kutukia hapa TZ  katika baadhi ya tawala hasa zilizo mtanguliza MUNGU na kumhubiri bila woga, HAKUNA tatizo linalo weza kutatuliwa kibinadamu isipokua MUNGU ameruhusu, wakati wa tawala iliyo pita Mungu alionekana kipekee hadi ulimwengu mzima ukatushangaa, nakumbuka ilitolewa ramani mpya ya dunia na tasisi moja marekani ikionesha duia nzima imechafuliwa na ibilisi isipokua Tanzania sehemu yote ya ramani ilionekana nyekundu ila TZ ilionekana nyeupe. wakati wengine wanahangaika kutatua kibinadamu sisi tuli hangaika kumkabidhi Mungu ashugurike na tukawa salama, akili ya mlevi sikuzote haimkubali MUNGU bali inajikubali yenyewe. ukifuata akili ya mlevi huongoza sikuzote katika uharibifu. 

bei ya mafuta kupanda ni kuwakandamiza watu wote. wenye maisha ya chini na maisha ya juu, wanao athirka sana ni wale wenye maisha ya chini yaani walio na kipato kidogo. vijiji vingi vya tanzania japo kuna umeme kwa sasa lakini bado wanatumia sana mafuta ya taa kuleta nishati ya mwanga na kupikia, ndio maana biashara ya majiko ya mafuta ya taa ipo sokoni hata sasa, hata mimi na tumia, kuongezeka kwa nauri kwa baadhi ya miji ndani na nje ya miji kunawaumiza wale wa kipato kidogo sana, nimeona kwa sasa kunaongezeko la watembea kwa miguu barabarani wakienda kwenye shuguri zao inamaana bajeti zao za kupanda daradara na bajaji au bodaboda zina goma. pia inawalazimu hawa wakipato kidogo wapunguze hata mizunguko kwa siku kwa kuhofia kutumia pesa nyingi katika usafiri, jambo hili limekuwa likipunguza kasi ya mzunguko wa pesa mtaani, kuongeza bei ya mafuta ni kumlimiti mwanachi shughuli zake hii husbabisha uchumi kukua taratibu au hata kuanza kushuka, haya ni maamuzi ya walevi, wanaagalia leo tu kesho hawaioni. faida ya leo hasara ya kesho hawaioni, 

wangeongeza kodi katika vileo ili wanywaji wapungue hii ingeondoa na kupunguza vilaza wengi katika jamii yetu, vichaa wanaongezeka kwa sababu ya ulevi na matendo ya ufedhuli yame kithiri. unapokunywa pombe nisawa na kunywa roho ya uovu, ndani ya pombe kumejaa kila aina ya uchafu.  

nakusihi mtanzania mwenzangu chunga sana milango ya fahamu inayo kupeleka kuzimu, 



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU