aliye tumwa kuwakomboa watoto wa shule naye atekwa..

 

Watekaji nyara nchini Nigeria wamemkamata mwanaume aliyetumwa kupeleka malipo ya fidia ili kuachiliwa kwa makumi ya watoto wa shule waliotekwa nyara.

Mzee huyo alitumwa na wazazi wa watoto hao baada ya kufanikiwa kukusanya naira 30msawa na (dola 73,000; Pauni 53,000) kwa kuuza ardhi na mali zingine.

Lakini wameachwa wakiwa hawana matumaini kufuatia utekaji nyara wake.

Kaskazini mwa nchi hiyo kuna wimbi la utekaji nyara shuleni unaotekelezwa na wahalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Mara nyingi katika matukio kama hayo fidia hulipwa lakini hii ni kesi nadra ambapo mtu aliyebeba pesa iliyokuwa fidia na kuwapelekea naye pia ametekwa nyara.

Watekaji nyara walimpigia simu mwalimu mkuu wa shule na kusema kwamba pesa zilizotolewa sio kiwango walichokubaliana.

Wanafunzi 136 walitekwa nyara kutoka shule ya Kiislamu huko Tegina, jimbo la Niger, mwishoni mwa Mei.

Watu wenye bunduki waliokuwa wamepanda pikipiki walivamia mji huo na kuanza kufyatua risasi kiholela na kumuua mtu mmoja huku mwingine alijeruhiwa.

Wakati watu wanatoroka,watekaji nyara hao walikwenda shuleni na kuwakamata watoto hao.

Wazazi na wasimamizi wa shule walijadiliana na wahalifu na wakakubali kulipa fidia.

Waliuza sehemu ya ardhi ya shule hiyo na mali zingine.

Mwalimu mkuu Malam Abubakar Alhassan anasema kuwa watu sita walitumwa na kiwango sahihi ili kukutana na watekaji nyara karibu na msitu ambao watoto wamashikiliwa.

Walipofika, wale watu wenye silaha walimtaka mmoja wa kikundi hicho, mzee, awafuate msituni ili pesa zihesabiwe.

Lakini baadaye walipiga simu kusema pesa hizo hazitoshi.

"Wazazi sasa hawajui hatma ya tukio hilo. Wanasema hawawezi kuchanga pesa zaidi na sasa wanamtegemea Mungu",

Zaidi ya wanafunzi 1,000 wametekwa nyara kutoka mashuleni huko kaskazini mwa Nigeria tangu Desemba mwaka jana.

Mamia yao bado hawajaachiwa huru lakini watoto 28 kati ya 121 waliochukuliwa kutoka Shule ya upili ya Bethel Baptist katika jimbo la Kaduna mapema mwezi huu waliachiliwa huru Jumamosi usiku.

Mamlaka zinakosolewa vikali kwa kushindwa kwao kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini kote pamoja na kuongezeka kwa matukio ya utekaji nyara wanafunzi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU