MATUMIZI YAKO

 

Jitahidi matumizi yako yalingane na mapato yako wala yasivuke kiwango kinachotakiwa vinginevyo utakuwa na madeni au utaiba na mwivi ni mzigo kwa wengine. Angalia matumizi yako yasiingilie akiba yako ukashindwa kufika ulikokusudiwa.
Usiige maisha ya watu wengine au kujiweka daraja la juu kwa kuombaomba, huo ni upumbavu, bali ishi katika daraja lako. Jipime unatumiaje muda, fursa, nguvu na mapato yako. Kwa nini uishi nyumba usiyomudu wakati uwezo wako ni mdogo? Ishi kwenye nyumba yako hata kama siyo ya bati maana Mungu anatukuzwa kwa kilicho chako.
Waamini wana tatizo la kupenda vitu vya bure, ni kosa kubwa kupanga nyumba ya mtu bila kulipa. Wokovu ni bure, lakini siyo rahisi, una gharama na Yesu alikufa kwa ajili hiyo. Mtakatifu kama hana fedha, anaweza kusahau kama ameokoka; kwa hiyo pambanua mambo ya siku zote na yale maalumu ili ujue kipi cha kufanya kwanza.
Walawi 10: 8-10 "Kisha BWANA akanena na Haruni, na kumwambia, usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kisha, mpate kupambanua kati ya yaliyo matakatifu na hayo yaliyo ya siku zote, na kati ya yaliyonajisi na hayo yaliyo safi".
Usibebe mambo mengi yakakufanya ushindwe kufuata utaratibu wa matumizi ya mapato yako, vile vile usikope kwa matumizi ya kawaida yasiyo ya uwekezaji bila kuwa na utaratibu wa kurejesha mkopo huo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU