WAABUDUO

SOMO: WAABUDUO

 


 

Mwanzo 1:1-2 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.”

Hapo mwanzo tunamuona Mungu akiumba mbingu na nchi, yapasa tufahamu nadharia yetu ya ibada, nadharia yetu ni nini? Ni mwanzo, tukiufahamu mwanzo basi tunaweza kuabudu katika uhalisia wa Ibada. Biblia inasema hapo mwanzo Mungu, si Efatha, Josephat wala waabuduo bali hapo mwanzo tunamuona Mungu akifanya kazi ya uumbaji. Alichokiumba kilikuwa ni kitupu na kikiwa, hii inamaana kuwa hicho alichokiumba Mungu kilikuwa kinahitaji utimilifu.

Mwanzo 1:3 “ Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.”

Hapa tunagundua ibada ni Nuru, hii inamaana gani? Utimilifu, na ukamilifu ni mzuri. Tunapoabudu yapasa tuanze mwanzo na tujue nini kilitokea.

Lolote unalotaka kufanya hapa duniani ni lazima uanze mwanzo, ibada yako lazima ianze mwanzo usiabudu hovyo hovyo, weka msisitizo katika eneo la kuianza ibada yako na sio mwendelezo ili uweze kupata majibu ya maombi yako.

Luka 4:18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.”

Yesu alikuja huku duniani kwa kazi gani?

• “Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema” Yesu alikuja kuhubiri msamaha, msamaha ni nini? Ni kuwatoa waliokuwa wenye dhambi ili wafikie toba, hii ndiyo sababu ya Yesu kuja hapa duniani.

• “Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao” Kuwaondolea watu mapepo na nguvu ya dhambi, unapofanya hivyo maana yake unawaweka tupu yaani wasijazwe na chochote ili waweze kujazwa na Nguvu za Mungu. Dhambi ilikuwa imekujaza hivyo usingeweza kuona mapenzi ya Mungu, Yeye alikuja akatutafuta na kutufanya tuwe watupu kutoka katika hila za mapepo na dhambi ndio maana Yesu alikuja ili kukufungua na kukufanya uwe huru.

• Yesu alikuja ili kutupa Nuru “Na vipofu kupata kuona tena” Nuru itakufanya uone kile ulichopungukiwa na kuhitaji, Yesu alikuja ili kutufanya tuwe kamili ili tuweze kuona.

• “Kuwaacha huru waliosetwa,” Ili kwamba chochote kinachokushikilia lazima kikatiliwe mbali ili mapenzi ya Mungu yakamilishwe kwako. Mungu alikuumba wewe kwa kusudi lake na sio kwa kusudi la baba yako wala la bosi wako au mume au mkeo bali ni kwa kusudi lake.

Huu msingi wa ufahamu ndio wengi wanaukosa usipofaulu katika huu hautaweza kustawi haijalishi nini utafanya itakuwa ni bure tu kwa sababu hautendi katika chanzo chako.

• “Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” Unapokuwa huru sasa unaweza kutangaza. Baada ya kazi hizi ndipo sasa unaweza kuuona uzuri wa Bwana.

MSINGI WA KUABUDU:

Msingi wa ibada yako lazima uanze na kutengwa, Mungu akamwambia Musa “Nenda kwa Farao umwambie awaachie watu wangu ili waje waniabudu”, Ibada ni lazima iwe mahali ambapo mtesi wako hawezi kuwepo.

Isaya 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. ”

Hii inamaana gani? Hiyo njia ni safari ambayo mtu anaiendea ili kuabudu.

• Ukifika mahali pa kuabudu hautazuiliwa na chochote wala hakuna wa kukusumbua.

• Mwabuduo hajipiganii bali kuna anayempigania.

• Mwabuduo akiwa mahali analeta pumziko.

Yeyote anayekwenda kuabudu hawezi kupotea wala hawezi kuacha kumwabudu Mungu kwa sababu ya kitu, ambaye si mwabudu anapokwenda kanisani na akasikia watu wanamsema harudi tena kanisani, waabuduo hata uwasengenye na kuwasema kiasi gani kamwe hawarudi nyuma.

Mtu yeyote akishafika ibadani anakuwa na raha ya ajabu, tamani kuwa mahali pa ibada.

Isaya 35:9-10 “Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.”

Waabuduo ndio watu pekee walio na furaha juu ya vichwa vyao na sio moyoni mwao.

Upumbavu upo kwenye akili, akili ikiwa na uerevu, ufahamu, maarifa na hekima hicho ndicho kinaitwa kicheko, kwa maana mwenye hekima hauwezi kumdanganya chochote kwa sababu ana ufahamu. Waabuduo wana ukamilifu katika akili zao kwa sababu hiyo wanaijua jana yao, leo na hata kesho yao hivyo hawawezi kupotea.

Mwanzo 1:4 “Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.”

Mungu aliiona Nuru kwamba ni njema, hii inamaana gani? Inamaana ukamilifu ni mzuri.

Mwanzo 1:5 “Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.” Mwabuduo lazima afahamu tofauti kati ya Nuru na giza tangu mwanzo, ni lazima afahamu ni jinsi gani Mungu alivitenga hivi viwili, hivi vyote viliumbwa na Mungu kwa kusudi lake, hivyo yapasa ufahamu kusudi la Nuru ni lipi na kusudi la giza ni lipi, tafuta upate kujua wewe ni wawapi.

Katika dunia hii giza limeonekana kuwa na nguvu kuliko nuru, katika dunia hii inayotiwa nguvu na giza wewe kama mwamini utawezaje kuishinda? Kwa kupitia ufahamu.

Bibli inasema Danieli baada ya kutia ufahamu akili yake mbingu ilisikia maombi yake, ufahamu ni wa muhimu sana kwako wewe mwamini ili maombi yako yajibiwe. Leo hii ninawaona Wakristo waliookoka wananena kwa lugha mpya lakini ni maskini, wana magonjwa ya kila namna nashindwa kuelewa, inakuwaje giza na Nuru vinaishi pamoja? Je! wewe ni Nuru au giza? Kama ni Nuru kwa nini giza linakushinda?.

Mtu aliyetiwa nuru atakuwa sawa na, Zaburi 1:3 “Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.”

Tatizo ni nini hapa? Ni ufahamu, ufahamu unakaa ndani yako, amani inaishi moyoni, hekima inakaa kwenye akili yako si kwenye moyo, hekima na maarifa vinakaa kwenye akili yako na siyo ndani ya moyo wako, mahali ambapo hekima, maarifa na Amani vinakaa inamaana kuwa Mungu yupo hapo, sasa Mungu akiwepo ndani yako maradhi yanawezaje kukusumbua? Ajali, wachawi wala sumu haviwezi kukudhuru, kwa nini? Kwa sababu umefunikwa na uwepo wake.

Mwanzo 3:23-24 “Kwa hiyo BWANA Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.”

Baada ya dhambi maisha ya Uumbaji yalibadilika na kwa sababu ya hilo badiliko liliwafanya Adamu na Hawa kufukuzwa kutoka mahali ambapo Mungu aliwakusudia au aliwaumbia ili wawepo.

Baada ya dhambi Adamu na Hawa walifukuzwa nje ya mahali ambapo palikuwa ni makao yao ya kudumu; na mahali pale walipokuwa wakikaa pakawekwa walinzi katika mlango wa kuingilia. Unaweza ukaishi huku duniani ukipambana ili upate kula au kupata kitu wala usifikiri ni kwa sababu ya mtu bali ni kwa sababu ya Mungu, upo katika maisha ya aina hiyo ni kwa sababu ya Mungu na wala sio ibilisi.

Mwanzo 3:17-19 “Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”

Katika mstari huu kuna mambo kadhaa tunayaona;

• Kula kwako kwa jasho,

• Miiba itaota na utakula kwa uchungu.

MASHAURI YA ROHO MTAKATIFU.

Mwanzo 4:7 “Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”

Kuna mashauri matatu ya Roho Mtakatfu kupitia mstari huu:-

1. Tenda vyema kwa maana kwa wewe kufanya hivyo utapata kibali.

2. Dhambi iko ili kukufanya uteseke na kukufanya maisha yako yawe ya uchungu.

3. Kwa gharama yotote ile yakupasa uishinde dhambi.

MASHAURI YA MUNGU.

Isaya 1:18-19 “Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;”

Kuna Mambo Matatu hapa yapasa tujifunze.

1. “Njoni, tusemezane”: Mungu anakuita wewe ingawa umetenda dhambi lakini bado anakuita, bado kuna nafasi kwa ajili yako hivyo usibaki hapo ulipo na kulia. Jifunze kumsikiliza yule aliyekuita na usitake akusikilize wewe tu.

2. “Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji;”: Dhambi zako ni mbaya mno lakini kwake kuna kusafishwa na kukufanya ukawa bora tena.

3. ”Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;”: Ukifanya yale ambayo Mungu anasema yapo mema kwa ajili yako siyo ya Mbinguni bali ni ya ulimwenguni humu ambayo ibilisi anayatumia kuwapa watu wake. Ibilisi hana kitu chochote anachofanya anaiba tu kutoka kwako sasa kama wewe ukijitambua ibilisi hataweza kuiba chochote kilicho cha kwako.

Waefeso 2:10 “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.”

Mungu alipomuumba mwanadamu hakumkusudia huyo mtu kujua mabaya au dhambi, tuliumbwa katika nuru ndani ya Kristo na sio katika giza hii inamaana kuwa tuliumbwa wakamilifu.

Ibilisi alitaka kupata washirika na akampata Hawa na tangu siku hiyo akili ya mwanadamu iliharibika kabisa, Mwanzo 6:5 “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.”

Mawazo ndio chanzo cha matendo yako hivyo chanzo kikiharibikiwa lolote utendalo litakuwa ni la uharibifu.

Usiishi kama wanadamu wanavyotaka uishi bali ishi kama Mungu anavyotaka uwe.

MAOMBI.

Usiombe maombi ambayo ibilisi anakusukuma kuomba bali omba maombi ya kutaka kuuona Uwepo wa Mungu katika maisha yako. Usiombe maombi ya kusema Mungu nataka hiki na kile, bali taka Uwepo wake kwako na hayo mengine yatakujilia.

• Usiombe maombi ya kutaka Mungu akupe vitu bali muombe Mungu akukamilishe.

Zaburi 51:10 “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu”

• Mwambie Mungu nipe kuwa kama wewe, nipe kukuwakilisha wewe hapa duniani.

• Bwana nipe kufanya kwa usahihi ili niweze kuujenga Ufalme wako, ukitaka kufanya jambo lolote huku duniani mimi nipo tayari.

Mwambie Mungu ukitaka mwanadamu wa kukuwakilisha huku duniani mimi nipo, ukitaka mtu ambaye atakuwa mbeba pesa kwa ajili yako mimi nipo.

Rejea katika ufahamu wako na urejee katika nafasi yako, Mungu anakusubiri afunike utupu wako na kuondoa madhaifu yako hivyo usiombe maombi ambayo ibilisi anayafurahia bali omba maombi yanayo mfurahisha Mungu. Yesu aliomba kwa Baba yake na kusema, “Baba najua unanisikia na ninajua mimi na wewe ni mmoja na niko hapa nitukuze mwanao ili nipate kukutukuza wewe”, acha tuombe maombi kwa ukamilifu.

Ukifanya maombi ya aina hii muda si mrefu maisha yako yatabadilika.

Kwa jinsi unavyotamani kumwabudu Mungu ndivyo Mungu anatamani kuwa na wewe, kwa sababu unachopanda ndicho unachovuna, Mungu hadhihakiwi.

Zaburi ni kitabu cha waabuduo, ukikifahamu hichi kitabu basi utaabudu, kamwe hautang’ang’ana ili uabudu bali utajua ni kwa jinsi gani uabudu na Mungu kamwe hataacha kuwa pale ulipo kwa sababu tamanio lake na tabia yake ni kuwa pamoja na waabuduo; Yeye anatafuta kuwaona hao wanaoabudu, ana shauku na kiu mno ili awaone na awapate waabuduo halisi. Yeyote anayeabudu kamwe hawezi kuwa pekeyake.

Ayubu 1:1-2 “Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.”

Ni mtu mmoja pekeyake katika jamii hiyo ambaye alimpendeza Mungu kwa sababu ya ibada yake, kwa sababu ya hiyo ibada Mungu alimuita Ayubu mkamilifu. Kila siku Ayubu alikuwa katika ibada na alikuwa akimpendeza Mungu, ibilisi alikuwa anakasirika na kufikiria ni namna gani ampate. Hata ibilisi pia anamtafuta mtu anayeabudu ili amwabudu yeye.

Kadri unavyotamani kumwabudu Mungu ndivyo Mungu anavyotamani kuwa na wewe, maana upandacho ndicho uvunacho Mungu hadhihakiwi.

Zaburi ni kitabu cha waabuduo ukikielewa kitabu hiki basi utaabudu na kamwe hautahangaika kuabudu maana utajua kuabudu na Mungu hatakoma kuwa hapo ulipo maana tamaa na tabia yake ni kuwa nayo cha waabuduo; anatafuta kuwaona wale wanaomwabudu kwa sababu ana hamu na kiu ya kuwaona na kuwapata waabuduo halisi.

Yeyote anayefanya ibada hawezi kuwa peke yake.

Ayubu 1: 1-2 "Palikuwa na mtu katika nchi ya Uz, jina lake Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwenye haki, na aliyemcha Mungu, akaufanya uovu. ”

Kulikuwa na mtu mmoja katika jamii aliyempendeza Mungu kwa ajili ya ibada yake, kwa ajili ya ibada hiyo Mungu aitwaye Ayubu mkamilifu. Kila siku Ayubu alikuwa ibadani na alikuwa akimpendeza Mungu hii ilimfanya shetani akasirike na kuwaza namna ya kumpata.

Hata shetani anatafuta mtu anayemwabudu ili amuabudu.

Ayubu 2:1-2 “Tena kulikuwa na siku hao wana wa Mungu walipokwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao, ili kujihudhurisha mbele za Bwana. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi? Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.”

Mungu alikuwa akijivunia Ayubu, siku moja Mungu alikuwa katika mkutano na Lucifer alijihudhurisha katika mkutano huo, giza na nuru wote ni watumishi wa Mungu mmoja kwa mambo ya giza na mwingine kwa mambo ya Nuru kwa sababu wote waliumbwa na Yeye kulingana na Biblia.

Mithali 16:7 “ Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.”

Vyovyote giza lilivyokufunika siku ukiamua kumwabudu Mungu utaondolewa kwenye giza na kupelekwa katika Nuru ili umpendeze Mungu.

Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.” Hivyo giza pia lipo kwaajili ya mambo ya giza.

Mwanzo 1:14 “Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka;”

Nuru ipo ili kutenga siku, majira na miaka, vyote vinatengwa na nuru na giza, unaihesabu siku kwa kulihesabu giza na Nuru. Watu wanauliza kwa nini Mungu hakumfukuza ibilisi kutoka pale? Unapaswa kutambua kuwa giza lipo ili kuikamilisha siku; usipomjua Mungu huwezi kuishi hapa duniani kwa furaha bali utaishi kwa mashaka na hofu. Giza na nuru vyote vipo humu duniani sasa maamuzi ni yako unataka kuwa na yupi.

 

Ayubu 2:4-5 “Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.”

Mungu alimruhusu ibilisi kumjaribu Ayubu lakini Ayubu hakubadilisha tabia yake, tabia gani hiyo? Tabia ya ibada. Ibada ni tabia inayoumbwa na kitu unachokiamini, unachokitumaini na kukipenda, ibilisi aliharibu kila kitu kwa Ayubu akabaki yeye na mke wake tu, kwa nini? Ayubu alikuwa mkamilifu na aliendelea na tabia yake hiyo.

Mungu alimruhusu ibilisi kugusa kila kitu kwa Ayubu isipokuwa uhai wake, kwa miaka mitatu Ayubu hakuwa na amani, furaha wala kicheko lakini bado tabia yake ilikuwa ni ile ile. Waabuduo hawawezi kuburuzwa wala kubadilishwa na kitu chochote kile haijalishi wao ni kina nani.

Leo hii watu wanajiita waabuduo lakini wakiguswa na chochote wanaacha kwenda kanisani na kumwabudu Mungu, wao sio waabuduo bado hawamjui Mungu wao wana wokovu wa dharura kwa maana hauwezi kuabudu kitu usichokifahamu.

Je! wewe una wokovu wa dharura au ni mwabuduo halisi?

Ayubu aliendelea na tabia yake ya ibada ambayo ilimfanya Mungu ambariki tena, mwabuduo halisi unaweza kuchukua kila kitu kutoka kwake lakini vitarejea mara dufu.

 

2 Samweli 24:18-25 “Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Haya! Kwea wewe, ukamwinulie BWANA madhabahu penye kiwanja cha Arauna, Myebusi. Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, kama BWANA alivyoamuru……….”

Daudi hakufunga wala kuomba ili kukomesha tauni iliyokuwa ikiangamiza watu bali alichokifanya alikwenda Kuabudu, alimtolea Mungu dhabihu na ile tauni ikakomeshwa. Ni maradhi au magonjwa gani yanatesa familia yako au ni mambo gani yanatesa familia yako? Umeomba na kufunga lakini hakuna kinachotokea? Kama umekwisha kufanya kila kitu jambo la mwisho unalopaswa kufanya ni dhabihu ili kubadilisha hali.

Kama kuna tukio lolote katika familia yako au maisha yako, ikiwa hilo tukio lilikuja ama kuruhusiwa na Mungu mwenyewe haliwezi kubadilishwa mpaka umefanya Ibada, hakikisha unafanya Ibada ambayo itampendeza Mungu.

Ayubu 2:1-2 "Ilikuwa siku moja wana wa Mungu walikuja kujidhihilisha mbele za Bwana, Shetani naye akaja kati yao ili ajidhihilishe mbele za Bwana. Bwana akamwambia Shetani, Toka lini wewe? Shetani akamjibu BWANA, akasema, Toka kwenda na kwenda duniani, na kwenda juu na chini ndani yake. "

Mungu alijivunia Ayubu. Siku moja Mungu alikuwa kwenye mkutano na lucifer akajidhilisha kwenye mkutano huo, giza na nuru vyote ni watumishi wa Mungu mmoja, kwa vitu vya giza na mwingine kwa vitu vya nuru maana vyote vimeumbwa na yeye acco Rding kwa Biblia.

Mithali 16: 7 "Njia za mtu zikimpendeza BWANA, huwafanya adui zake kuwa na amani naye. "

Giza lolote lililokufunika, siku ukiamua kumwabudu Mungu ungetolewa gizani na kutumwa kwenye Nuru ili umpendeze Mungu.

Mithali 16:4 "Bwana amejitengenezea vitu vyote; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. "Kumbe giza pia lipo kwa ajili ya mambo ya giza"

Mwanzo 1:14 "Mungu akasema, Na iwe nuru katika anga la mbingu, zigawanye mchana na usiku; na ziwe ishara, na majira, na siku, na miaka;"

Nuru na giza vipo kutenganisha siku, majira na miaka. Unahesabu siku kwa kuhesabu Giza na Nuru. Watu huuliza kwa nini Mungu hakumtoa shetani nje? Lazima utambue kuwa giza lipo ili kukamilisha siku; usipomjua Mungu hutaweza kuishi duniani kwa furaha, utaishi kwa mashaka na hofu. Giza na nuru vyote vipo hapa duniani sasa maamuzi ni yako juu ya kile unachotaka kuwa nacho.

Fanya jambo kwa ajili ya ibada yako, mtolee Mungu kile unachokijua, kama una ujuzi fulani na unajua kuwa unaweza kutumika kanisani na ukasababisha kazi ya Mungu isonge mbele toa hicho na usisubiri kulipwa na Mungu akikuona hivyo kamwe hatakupungukia.

Kutoka 31:1-6 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza;”

Mungu amekuweka wewe ili ufanye kitu katika Ufalme wake hivyo usikae chini wakati unajua unaweza kufanya kazi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Kupitia akili yako, nguvu zako, mali zako onesha ibada yako kwa yule aliyekuumba.

Kama wewe una ujuzi wa IT ( Tehama) au Television tafuta watu wanaohusika katika hiyo sehemu hapa kanisani na ukamtumikie Mungu kwa kipawa chako alichokupa.

Kupitia kipawa alichokupa Mungu, je! Umemuabudu vipi Mungu wako kupitia hicho? Unakuta mtu anakwenda kanisani mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa kumi na mbili hakuna anachokifanya kanisani, ukimuuliza je! Amefanya watu wangapi wafikie toba? Hana, mtu wa aina hii sio muabuduo bali ni mnafiki.

Maarifa uliyopewa ni kwa ajili ya Mungu, hakikisha unatumia ujuzi wako kwa ajili ya kuujenga Ufalme wa Mungu na usisubiri kulipwa.

Ayubu 2: 4-5 "Naye Shetani akamjibu Bwana, akasema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyonayo mtu atampa kwa ajili ya maisha yake. Lakini tia mkono wako sasa, uguse mfupa wake na nyama yake, naye atakulaani uso wako. "

Mungu aliruhusu shetani amjaribu Ayubu lakini Ayubu hakubadili tabia yake, je tabia hiyo ni nini? Tabia ya kibinafsi. Ibada ni tabia iliyoundwa na kitu unachokiamini,kukiamini na kukipenda,shetani aliharibu kila kitu kwa ayubu na kumuacha yeye na mkewe peke yao,kwanini? Ayubu alikuwa sawa kabisa.

Mungu aliruhusu shetani aguse kila kitu isipokuwa maisha ya Ayubu. Kwa miaka mitatu Ayubu hakuwa na amani, hakuwa na furaha wala kicheko lakini bado tabia yake ilikuwa ile ile. Waabudu hawavutwi wala kubadilishwa na chochote hata kama ni nani.

Leo watu wanajiita waabudu lakini wakiguswa na jambo lolote wanaacha kwenda kanisani na kumwabudu Mungu, wakati hawamjui Mungu kama wana wokovu wa dharura maana huwezi kuabudu kitu usichokijua.

Je una wokovu wa dharura au wewe ni mwabudu halisi?

Ayubu aliendelea na mazoezi yake ya kidini ambayo ilisababisha baraka ya Mungu tena. Unaweza ukachukua kila kitu kutoka kwa mwabudu wa kweli lakini kitarudi mara dufu.

2 Samweli 24:18-25 "Na Gadi akamwendea Daudi siku ile, akamwambia, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi; Panda juu madhabahu, ukamwendee Bwana madhabahu katika uwanja wa Arauna, Myebusi. Naye Daudi akapanda katika neno la Gadi, kama Bwana alivyoamuru.......... "

Daudi hakufunga wala kuomba ili kupisha pigo lililokuwa linawaangamiza watu bali alichokifanya ni kwenda ibadani, alimtolea Mungu dhabihu na pigo likasimamishwa. Ni magonjwa gani au magonjwa gani yanaitesa familia yako? Je umeomba na kufunga lakini hakuna kinachotokea? Ukishafanya kila kitu cha mwisho unachopaswa kufanya ni kujitolea kubadilisha hali hiyo.

Kama kuna tukio lolote katika familia au maisha yako, kama tukio hilo lilikuja au lilitakaswa na Mungu mwenyewe na haliwezi kubadilishwa hakikisha unafanya Ibada itakayompendeza Mungu.

Usalama wa mtu anayeabudu umo ndani ya ibada kama ukitaka usalama mwabudu Mungu.

Kutoka 15:26 “Akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.”

Ukianza kuabudu hata kama una magonjwa ya aina gani yatatoweka kwako, kwa nini? Kwa sababu umeamua kuabudu na Mungu ataondoa hayo maumivu mbali na wewe, usalama wa maisha yako umo ndani ya ibada.

Kutoka 23:20-23 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea. Jitunzeni mbele yake, mwisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake……..”

Ukiamua kuabudu hakuna cha kukudhuru, adui zako wote watamalizwa hata umaskini. Je unataka kuondokana na umaskini? Mwabudu Mungu katika Roho na kweli.

 

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU