#SOMO la leo 20/08/2023 na Mtu wa MUNGU Nabii BG Malisa.
▪︎LUKA 19:29-30
Unaweza ukawa unaishi mahali flani lakini katika ulimwengu wa roho umefungwa kijijini kwenu.
Kijiji chenu ndiyo chimbuko lenu, ndiyo asili yenu. Huwezi kufanikiwa zaidi ya asili ya kijiji chenu.
▪︎Kule ulipotoka ndiyo chimbuko lenu, ndipo historia yenu ilipo, huwezi kwenda zaidi ya chimbuko lenu, inahitaji ukombozi na kufunguliwa kwa kiwango cha juu ili ufanikiwe.
Kumbuka: NI LAZIMA URUDI UCHUNGUZE ASILI YA KIJIJI CHENU NA UISHUGHULIKIE
▪︎Ardhi ya kijiji chenu inahitaji ukombozi wa hali ya juu, watu wengi wapo mjini wanapambana kutafuta mafanikio, wanatafuta upenyo na hakuna chochote kinachotokea, pasipo kujua kuwa msingi wa maisha yao unategemea kule walipotoka. Tambua na uelewe kwamba kuna siri kubwa iliyojificha katika ardhi ya kijijini kwenu.
▪︎MARKO 8:26.
Kuna matatizo mengine yanatokana na maeneo ulipotoka, katika kijiji chenu kuna maagano yalifanyika yakakushikilia mpaka leo. Kuna matatizo mengine siyo ya kuombewa tu bali unatakiwa kwenda na kuikomboa nafsi yako kabisa.
▪︎Matatizo makubwa yanahitaji nguvu kubwa na maombi makubwa, unahitaji kushughulikia hicho kijiji yaani mahali ulipotoka, unatumia nguvu kubwa kufanikiwa tambua kuwa kuna mahali umeshikiliwa ambapo ndipo ulipotoka, zipo madhabahu za ukoo zimekufunga zinakupeleka usipotaka. Shughulika na hizo madhabahu utaona upenyo.
▪︎Kijiji chenu kinaweza kukuwekea mpaka, jaribu kuchunguza hata watu wa familia yenu ni watu wa aina gani, wanafanya nini? Utagundua ni watu ambao mnazunguka katika mzunguko unao fanana.Kwasababu umefahamu siri hii,anza maombi ya nguvu na wewe hautakuwa kama wao katika Jina la Yesu Kristo.
▪︎Madhabahu za kijijini kwenu zinakushinda kwasababu zimetolewa sadaka, madhabahu yoyote ya giza ili ifanye kazi lazima kuna sadaka inatolewa, usitegemee kuvunja madhabahu bila sadaka yoyote ya ukombozi
Kwa mfano-: Ukilala usiku unaota ndoto upo kijijini kwenu, ili utoke kwenye hichi kifungo lazima utoe sadaka ya Ukombozi yaani ukomboe nafsi yako mahali ilipofungiwa.
▪︎Ili ushinde hizi madhabahu za ukoo lazima utambue nguvu inayoshinda hiyo madhabahu
Nguvu ya kushinda madhabahu za ukoo ni SADAKA.
Maoni