TUNDA LA ROHO

 Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria."

- UPENDO 

Hili ni tunda la kwanza la Roho, Yesu Kristo wakati akitembea watu wengi walimfuata kwasababu alikuwa na Pendo la kweli ambalo ni tunda lililosababisha watu kumfuata kila alipo pita, Pendo linamvuta mtu kuja karibu yako, hivyo katika kanisa ni lazima kuwa na tunda la upendo ili kusababisha ukombozi wa watu. 

- FURAHA

Furaha inajengwa na Pendo, kama kanisa furaha inasababisha umoja na ushirikiano na inasababisha ukombozi kwetu. 

- AMANI

Amani ni kila kitu katika maisha, pasipo amani hakuna mafanikio. Ndani ya amani kuna utoshelevu kwa kila jambo. 

- UVUMILIVU

Uvumilivu na tabia ya Mungu , kama Mungu wetu anaweza kutuvumilia na sisi pia tunapaswa kuwa wavumilivu kwa kila jambo

- UTU WEMA

Utu wema ni kuwaza mema juu ya mtu mwingine

-FADHILI

Fadhili ni ile hali ya kujitoa kwa ajili ya mtu Fulani pasipo kujali kitu chochote

- UAMINIFU

Katika maisha tunapaswa kuwa waaminifu kwa kila hali, ni lazima kujenga uaminifu katika kila sehemu, uaminifu unaanzia nyumbani na kwa watu wanaokuzunguka. Pia kazi ya Mungu inafanywa kwa uaminifu. 

- UPOLE 

Upole sio wa kutembea bali ni upole wa matendo na tunapaswa kuwa na upole.

- KIASI

Kuwa na kiasi kwa kila jambo, usifanye mambo kwa kupitiliza kwasababu pasipo kiasi kuna uharibifu. Matunda haya yote ndiyo yanayosababisha ukombozi kwa mtu na hata kwa kanisa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU