UJUMBE WA ROHO.
Nalikuwa katika njozi NAMI nikaona tazama watu katika mji wangu wakienndelea na shughuli zao, Lakini wanadamu wote tunaonekana tunanamchukulia MUNGU YEHOVA na IBADA ZAKE kuwa kitu Cha kawaida, inaonekana hakuna injiri ya kweli Kwa wanadamu wa muda huo.
Basi ilikuwa ni siku iliyo Anza vizuri sana, Jua la ASUBUHI liliangaza vyema bila kuwepo hata wingu Moja,
Ilionekana hakuna mvua inaweza kunyesha siku hiyo.
Watoto walikuwa wakienndelea na michezo Yao huku watu wazima wakiendelea na shughuli zao,
GHAFRA ,.
YAANI KUFUMBA NA KUFUMBUA
milimani ikaonekana wingu na dhoruba Kali ambayo hapana mtu akikutwa nayo anaweza kupona,
Dhoruba Kali ilikuwa inakuja mjini kwetu Kwa Kasi isiyowezekana kuikimbia. Watu wa mji walionekana wakikimbia kila mmoja aiokoe nafsi yake bila hata kuwakumbuka watoto wao na ndugu na jamaa zao.
NAMI nilitaka kukimbia lakini nikawaona wanagu wadogo wakiwa wame duwaa Wanashangaa Ile tufani Kwa huzuni.
Nikajiuliza inamaana hata mama Yao kwaacha?
Basi nikaenda nikawashika MIKONO nikaanza kuwahimiza tukimbie wanangu kama tunakufa tutakufa tukiwa wote...........
Roho akaanza kunishuhudia wakati tunakimbia kuwa wakati wa dhiki kuu ukaribu.
Roho akanionesha ulimwengu mzima kuwa wanadamu wote wanashuhudia hiyo dhoruba na sio katika mji wako tu. Wanadamu wote ulimwenguni wanakimbia kama mnavyo kimbia nyie.
Una HERI wewe uliye yaona HAYA siku chache kabla hayajatukia.
Uovu kwenu Kwa Sasa ni kitu Cha kawaida. IBADA Kwa MUNGU YEHOVA ni kitu Cha kawaida kwenu.
Mkiendelea hivyo hakuna atakae salia hapa ulimwenguni
Bwana anataka kuusafisha ulimwengu ili uwe mpya kwaajiri ya kutimiza mapenzi yake aliyo ikusudia Dunia hii.
Mbingu mpya na nchi mpya.
Tubuni na kuiamini injiri ya kweli maana ufalme wa mbingu na nchi mpya umekaribia.
Yesu Yu karibu mawinguni.
Dhoruba Kali ya moto ikaribu.
Mvua ya mawe mazito ya Tani Moja Iko karibu sana.
Kwakuwa nawapendeni wanangu
Huu ni mwaka wa Toba ya machozi na uamsho mpya wa ki Mungu Kwa wanadamu wote duniani.
🙏 Itaendelea..
Maoni