Machapisho

Nguvu ya Mwamini.

  Nguvu ya Mwamini. 2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”   Hauhitaji kukumbuka ya jana kwa maana yamekwisha, ni kwa nini haupokei kutoka Mungu? ni kwa sababu wewe unawaza ya jana. Mungu hana mpango wa jana yako, kwa nini? Kwa sababu jana ni ya kale na imepita, Mungu anampango na nini? Mungu anampango na leo na kesho yako, Mungu ana shauku mno na kesho yako, kama unataka kutembea na Yeye zingatia mapenzi yake, mapenzi yake sio jana yako bali mapenzi yake yapo katika kesho yako. Kama upo ndani ya Kristo na umezaliwa mara ya pili yaani umeokoka Mungu anashauku sana na wewe, anasema jana yako imepita. Jana ni mambo ya kale, je ni nani anaye zingatia mambo ya kale? Tunatumia vitu vya kale kwa ajili ya kuvitazama tu tunaenda katika makumbusho ili kuona vitu vya zamani tu, hauzingatii sana vitu vya kale. Kwa nini unampango sana na jana yako wakati jana yako imepita, ilihali hata nguo zako za j...

UHUSIANO WA MAGONJWA NA DHAMBI;

Picha
  UHUSIANO WA MAGONJWA NA DHAMBI; (1) NGUVU YA ISHARA NA MAAJABU (YOHANA 4:46-48) Tunaona hapa Yesu akimwambia diwani mwenye mtoto mgonjwa, “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa?” Ishara, maana yake tendo lolote linalodhihirisha kwa dhahiriUWEZO WA MUNGU. Maajabu, ni mambo yanayofanywa na Mungu, yanayomfanya mwanadamu kupigwa na mshangao, kwa kuwa ni tofauti na desturi au taratibu za kibinadamu. Ishara na maajabu, yana nguvu ya ajabu katika kuihubiri Injili kwa utimilifu. Wako watu wengi leo katika ulimwengu huu ambao, kama diwani huyu, hawawezi kumwamini Yesu, wasipoona ishara na maajabu. Diwani huyu, alimwamini Yesu, yeye na wote wa nyumbani mwake, kutokana na ishara na maajabu aliyoyaona YOHANA 4:52-53. Huyu, ni mmoja kati ya watu wengi walioamini baada ya kuona ishara na maajabu YOHANA 2:11, 23; 7:31; MATENDO 13:12. Watu wengi ambao hawajaokoka, watajengewa utayari wa kutusikiliza ikiwa wataona ishara na maajabu MATENDO 8:6. Siyo hilo tu, ni rahisi kwa watu wengi kuthib...

Dhiki kubwa

Picha
  Dhiki kubwa Tunajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele saba. ( i ). Dhiki tofauti na zote ( ii ). Muda wa dhiki kubwa ( iii ). Majina yanayotumika kuzungumzia dhiki kubwa ( iv ) Watakaohusika kuileta dhiki kubwa ( v ). Makusudi ya dhiki kubwa ( vi ) Hali itakavyokuwa wakati wa dhiki kubwa ( vii ). Jinsi ya kuikwepa dhiki kubwa ( I ). DHIKI TOFAUTI NA ZOTE Wanadamu hapa duniani, wanapitishwa katika dhiki za namna namna. Wanapitishwa katika mateso ya namna namna. Wengine wanapitishwa katika hali nzito ya njaa nchi nzima hali inakuwa mbaya. Nchi ambazo zimewahi kushuhudia njaa kali kama Ethiopia na Somaria, watu watakondeana na kubaki mbavu kabisa. Njaa itakuwa kali kiasi kwamba hata ukipita mjusi watatamani kuurukia waweze kuula lakini hata nguvu za kuurukia mjusi zinaweza kukosekena . Watu wengine watafukiwa na vifusi sehemu zile za India kutokana na matetemeko. Wengine wataweza kupelekwa mbali kwa kurushwa na vimbunga. Dhiki ulizozipata kwa kuanguka katika mapo...