HABARI YA MSALABA.

HABARI YA MSALABA. Tuko Kanisani kwa sababu ya imani yetu tuliyonayo na hatupo ili kusheherekea, tunakusanyika hapa kwa ajili ya imani ya Yesu Kristo ambayo ilianza na Ibrahimu, ni imani gani hiyo? Ya kumwamini muumbaji. Kama Biblia inasema “pasipo imani hauwezi kumpendeza Mungu” njia pekee ya kumpendeza Mungu ni kukaa katika imani; kwa nini watu wanahangaika, wanateseka na wanang’ang’ana ili wapate chakula, wapate kodi au ada ya shule? Kwa sbabau wamekosa Imani ndani yao. Wafilipi 4:13 “ Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. ” Yupo Mungu anayekuwezesha kupata kile unacho kihitaji, lakini kama haumtumaini kamwe hautaweza kuishi vizuri hapa duniani. Imani inamfanya mtu jinsi alivyo, je! Wewe unaamini nini? Tutayaona maisha yako. Imani tuliyomo ndani yake inaanzia pale msalabani na siyo mahali pengine. Ukitaka matatizo, mateso na maumivu yote yafikie kikomo ni pale utakapolijua Neno msalaba. 1 Wakorintho 1:18-19 “ Kwa sabab...