
Historia ya Wokovu Jinsi Pietro Perugino alivyochora Mateso ya Yesu msalabani kwa mtindo wa Stabat Mater , yaani akiwa na Bikira Maria na Mtume Yohane chini yake ( 1482 ). Kifo na ufufuko wa Yesu ndiyo kilele cha historia ya wokovu kwa imani ya Ukristo . Kwa jina hilo Wakristo wanamaanisha ufafanuzi wa mpango wa kazi ya Mungu kwa wokovu wa binadamu kadiri ya Biblia . Yaliyomo 1 Maana ya historia 2 Maana ya wokovu 3 Imani kuhusu Biblia 4 Agano la Kale 4.1 Vitabu vitano vya Torati 4.2 Uumbaji 4.3 Dhambi ya asili 4.4 Watu walivyoishi baada ya dhambi 4.5 Nuhu 4.6 Mnara wa Babeli 4.7 Abrahamu (1900-1800 hivi K.K.) 4.8 Watoto wa Isaka: Esau na Yakobo 4.9 Yosefu na ndugu zake kushukia Misri (1700 hivi K.K.) 4.10 Utumwa wa Misri na wito wa Musa (1250 hivi K.K.) 4.11 Mapigo ya Wamisri 4.12 Safari ya kuendea Nchi ya ahadi 4.13 Agano la Mlima Sinai 4.14 Ndama ya dhahabu 4.15 Mungu kujifunua ten...