Uzazi wa mpango kwa kutumia njia za asili
Open main menu Uzazi wa mpango kwa njia asilia Lugha Download P Uzazi wa mpango kwa njiap asilia maana yake ni mbinu zile za kuzuia mimba isipatikane katika tendo la ndoa ambazo zinafuata maumbile tu. Njia asilia za kupanga uzazi ni mbinu ambazo hazihusishi vifaa wala kemikali , bali zinategemea ufahamu wa uwezo wa mwanamke kupata au kutopata mimba wakati wa kufanya tendo la ndoa. Wanawake ambao wananyonyesha na wanapenda kukwepa mimba wanaweza kufanya tendo la ndoa kwa kutegemea kukatizwa kwa hedhi wakati wa kunyonyesha. Mbali ya huo ujuzi wa jumla, uzazi unaweza kupangwa kwa kutofanya tendo la ndoa siku 13 hivi ambapo katika mzunguko wa hedhi kuna uwezekano wa kupata mimba. Kinyume chake wanandoa wanaweza kulenga uzazi kwa hakika zaidi wakifanya tendo la ndoa kwa kutumia vizuri siku zinazouwezesha. Vilevile wanaweza kuchagua...