JINSI YA KUMSHINDA SHETANI
JINSI YA KUMSHINDA SHETANI. sehem ya 1. Bwana Yesu asifiwe wapendwa. Bwana YESU amenipa wakati mzuri Mimi Jacob Wa kunieleza Na kunifunza jinsi Na namna ya kupigana vita vya kiroho. Na ameniahidia kua kila asomaye Na atakaye nisikiliza kwanjia yoyote ile atakombolewa. Jifunze kupigana vita vya kiroho kwa upana Mkubwa zaidi. Katika makala zangu utajifunza kushindana Na kushinda. Huwezi kushinda vita yoyote kama huna ujuzi wala mbinu za kupigana Na adui. Pia lazimaujue mbinu za adui unaye pigana naye, aina ya silaha anazo tumia, nguvu ya jeshi lake Na niwakati gani adui huwa anashambulia. Nijambo la ajabu sana watakatifu Wa Mungu wao humchukulia shetani kama kitu cha kupuuza tena kinyonge Na kisichokua Na uwezo wala maarifa. NISAWA LAKINI NIHATARI SANA KWA UPANDE MWINGINE. Mtu Wa Mungu elewa kwanza unapigana Na shetani ambaye Alisha hukumiwa. Hana nafasi tena ya kutubu. Tena unapigana Na shetani ambaye amepewa ulimwengu huu, anaitwa mkuu Wa Giza ...