KIFO KWA MTU ALIYE ZALIWA MARA YAPILI
.jpeg)
KIFO KWA MTU ALIYE ZALIWA MARA YAPILI Kuna mambo mengi sana ya kujifunza katika Kitabu cha YOHANA. Leo, tunaendelea kujifunza Kitabu hiki katika Biblia zetu, kwa kutafakari kwa makini YOHANA 11:1-16. Katika mistari hii, tunasoma juu ya kifo cha Lazaro, na hivyo kujifunza juu ya KIFO KWA MTU ALIYE ZALIWA MARA YAPILI . Hata hivyo, kuna mafundisho mengi yanayoambatana, tunayojifunza hapa. Tutayagawa mafundisho tunayoyapata katika mistari hii, katika vipengele kumi na moja:- (1) UPENDO WA KINDUGU KATIKA UGONJWA (2) KUUGUA KWA WATU WALIOOKOKA (3) UGONJWA HUU SI WA MAUTI (4) UTUKUFU WA MUNGU HUONEKANA KATIKA MATATIZO (5) UPENDO WA MUNGU KATIKA KUCHELEWA KUSHUGHULIKA NA MATATIZO YETU (6) KUSAMEHE NA KUSAHAU (7) MTU AKIENDA MCHANA HAJIKWAI (8) YESU KWETU NI RAFIKI (9) KIFO CHA MTU ALIYEOKOKA (10) UWEZEKANO WA WANAFUNZI WA YESU KUTOKULIELEWA NENO LA MUNGU (11) WAJIBU WA KUTIANA MOYO KUSONGA MBELE (1) UPENDO WA KINDUGU KATIKA UGONJWA Lazaro alikuwa hawezi, yaani ali...