KUFUNGA
KUFUNGA: Nini maana ya kufunga?
Isaya 58:6-14 “Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu,
kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila
nira? Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini
waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala
usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapopambazuka
kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu
wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde…….”
·
Kufunga maana yake ni
kuachilia matendo maovu.
·
Kufunga ni kukusababisha
wewe kutimiza mapenzi ya Muumba wako,
·
Kufunga ni kumwambia
Mungu mimi sistahili pasipo wewe, yaani inamaana ni kumkaribia Mungu.
·
Kufunga ni kuuita uwepo
wa Mungu uwe pamoja nawe na kutembea na wewe, uwepo wake ni utukufu wake na
utukufu wake ni ulinzi wako. Hivyo unapo funga ni sawa na unauambia utukufu wa
Mungu uje kwako.
·
Unapo funga ni sawa na
unamwambia Mungu mimi sina nguvu dhidi ya maadui zangu ninahitaji usaidizi
wako.
·
Ni kumruhusu Mungu atende
jambo kwa niaba yako sawa sawa na kile ulicho mueleza.
Kufunga ni jambo lenye nguvu kwa maana unamuhusisha Mungu katika
maisha yako hivyo lolote utendalo utastawi. Unapo funga inamaana kuwa umeamua
kuutiisha mwili wako uwe dhabihu iliyo hai mbele ya Mungu. Ni kumwambia Mungu
mwili huu ni hekalu lako, utakapofanya hivyo maana yake utakuwa unaua maradhi
na magonjwa katika mwili wako, kwa maana uwepo wa Bwana unakuwa ndani yako na
magonjwa hayawezi kukaa katika uwepo wa Mungu. Kufunga maana yake ni kuiambia
dunia kuwa umasikini hauna nafasi kwangu kwa maana uwepo wa Mungu upo
ndani yako. Ni kuruhusu kutumiwa na Mungu.
Unapo funga tarajia jambo la pekee kutokea katika maisha yako.
Mfalme Yehoshefati alipokuwa na watu wake alitangaza kufunga kwa watu wake wote
na baada ya hapo neno likamjia na kumwambia 2 Nyakati 20:15 “akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi
mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope,
wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; KWANI VITA SI YENU BALI NI YA
MUNGU.” kufunga maana yake ni kugeuza vita iwe si yako
bali iwe ni ya Bwana, unapo funga unabadilisha jinsi ulivyo.
Ni muhimu sana kwako wewe kuelewa maana ya kufunga, kufunga sio
kupunguza kula chakula, usifunge na siku nzima ukakusanya chakula kwa
ajili ya jioni, huu sio mfungo bali umebadilisha tu saa za kula. Baada ya
mfungo Yehoshefati hakupigana bali alipofika vitani akakuta maadui wameshapigwa
na ye akateka nyara tu, mfungo unakusaidia wewe kupata vitu ambavyo
haukutarajia kuvipata.
IMANI
1 Yohana 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku
ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.” Imani inaweza kupatikana kwa wale waliozaliwa na Mungu na si
wale waliozaliwa na mwanamke. Hii inamaana kua kwa wale waliozaliwa
naYesu inamaana wamezaliwa katika roho hawa ndio unaweza kukuta imani ndani
yao.
Mshiriki wa imani maisha yake yanaonekana hapa: 1 Yohana
5:18 “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na
Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu
hamgusi.” aliye zaliwa na Mungu hatendi dhambi, dhambi hairuhusiwi kwake
na pia anajilinda na kujitunza kwa nini au anatunza nini? Hasubiri kuambiwa
usifanye hiki na kile bali yeye anajitunza na kujilinda mwenyewe, hii
inamaana kuwa anatunza maisha ya Mungu ndani yake na si kutunza nguo au nyumba
yake. Kujitunza mwenyewe ni pamoja na kumtunza mkewako na watoto, nyumba yako,
kazi yako na biashara yako. Watu wa imani hawana hofu kwa sababu ibilisi hana
nguvu juu yao, mara zote ibilisi anawaogopa. Yeyote anaye enenda katika imani
yeye ni mshindi na anatembea katika ushindi kamwe ibilisi hawagusi.
Nini maana ya imani? Imani maana yeke ni:-
·
Imani ni kutumaini si
katika uwezo wa wanadamu, sio kusema labda inawezekana, labda itakuwa, bali
imani ni kweli.
·
Imani sio hoja ambayo
inakuja kwa kufikiri, kupitia mtazamo wako wala katika namna yako ya kufikiria.
·
Imani maana yake kile
Mungu amesema ni kweli, unapojua kile Mungu alichosema kuwa ni kweli hiyo ndiyo
inaitwa Imani.
·
Imani huja kwa kusikia
Neno na kuakisi katika ahadi za Mungu aliye juu yeye aliyesema na kile anacho
kisema ndicho anachokitenda. Hakuna kitu kinacho mzuilia Mungu huku duniani.
Imani mara zote ipo katika Neno la Mungu, unapo litendea kazi neno
inamaana kuwa unatenda katika imani; Biblia inasema “imani haiwezi kushindwa” hivyo inamaana kuwa ukitenda katika neno hautakaa
ushindwe.
Mungu atakufurahia pale utakapokuwa katika imani, hii inamaana
kuwa ukiwa katika Neno Mungu atakufurahia na ndio maana yeye akasema “naliangalia neno langu ili nipate
kulitimiza” ukitenda katika Neno unampendeza Mungu kwa sababu yeye
analiangalia Neno lake. Nani aliye na Neno? Muabuduo, Je! Wewe ni
muabuduo? Kama wewe ni muabuduo Mungu anakuangalia na kukuangalia wewe.
Mungu yumo ndani ya Neno. Analipenda analiishi na kulitendea kazi Neno. Ukiwa
ndani ya Neno mara zote wewe ni mtendaji; Unaweza kutenda lolote
unalopaswa kutenda.
Ayubu 22:28 “Nawe
utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako.” Ukitenda sawa sawa na Neno unaishi katika Neno na ndipo
utaamrisha chochote nacho kitakuwa, utakaposema nataka kujenga hauhitaji pesa
bali unahitaji Neno ili hilo jambo lipate kutimia kwako.
Baba wa mbinguni anasubiri kulitendea kazi Neno lake, unapo
lisoma Neno, utakapo litamka na kuliishi hilo Neno inamaana kitu chochote
utakacho kitamka kitakuwa kwa maana Neno linaishi ndani yako. Kwa maana hiyo
neno lolote utakalo litamka litatoka na nguvu ya Mungu kwa sababu neno linaishi
ndani yako.
Wengi wenu mnatafuta tafuta mistari ya Biblia pasipo kulijua
Neno lililo tamkwa. Yesu aliwatuma wanafunzi wake waende ili kuwafanya watu
wawe neno lililo tamkwa. Wakikubali inamaana na wao wanakuwa neno lililo tamkwa
na wakitembea wanakuwa hilo Neno na lolote watakalo tamani litakuwa
kwao.Ukitembea katika Neno lililo tamkwa tangaza lolote nalo litatokea kwako.
Ukiri: Baba
mimi ni Neno lililo tamkwa, nitatamka sawa sawa na jinsi nilivyo lazima
nidhihirike ili kwamba ninapo tamka chochote lazima kidhihirike kwangu kwa jina
laYesu.
Maoni