KWANINI TUNAFUNGA NA KUOMBA
Kwa nini tunafunga? Ni sawa na tunamwambia Mungu kuwa tunataka
kurejea kwako, tutembee na wewe na tuwe na wewe, kwa kusudi gani? Ili tupate
KUSTAWI.
NINI MAANA YA USTAWI?
·
Ni maisha ya kumeondokana na uhitaji yaani ni maisha ya
utoshelevu,
·
Ustawi maana yake ni utimilifu wa mtu, pasipo ustawi bado
haujatimia.
·
Ustawi maana yake umeufikia wito ambao Mungu amekuumbia, Mungu
alimuumba mwanadamu kwa sura na mfano wake, kwa kusudi gani? Ili afanane naye.
Katika Mungu hakuna labda labda bali kuna utimilifu.
Biblia inasema nini kuhusu Ayubu? Ayubu alikuwa mtu mkamilifu,
nini maana ya ukamilifu? Maana yake alikuwa ni mtu aliyestawi. Alikuwa na
watoto, wanyama na watumwa walio mzunguka wa kiume na wakike, ustawi maana yeke
ni utimilifu wa mtu. Ayubu 1:1 “Palikuwa na
mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa
mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.”
Unapo sema mtu huyu ni mkamilifu inamaana ameweza kufikia chanza
cha kuumbwa kwake.
Ustawi maana yake ni kufikia mwisho yaani kufikia utimilifu wa
maisha
Ustawi maana yake ni kufikia kilele cha maisha yako, kama
haujafikia hicho kilele inamana kuwa haujastawi bado.
Isaya 1:19 “Kama
mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;” Hii inamaana kuwa
ukikubali na kutii ndipo utaweza kufikia katika mraba wako, kila mtu ana mraba
wake wa kupiga mbio ili kufikia ustawi wake.
Ustawi si kwa ajili ya mtu fulani tu, la! Bali ni kwa kila mmoja
aliyeumbwa na Mungu, kwa nini wengine wanastawi na wengine hawastawi?
Inategemeana na mitazamo yao.
Chanzo cha uovu wote huku duniani ni watu kupenda pesa, tatizo
si pesa bali ni wanadamu wanapenda pesa.
Ustawi maana yake ni pesa inakupenda wewe yaani uumbaji
unakupenda. Haujaumbwa ili uupende uumbaji bali ni uumbaji ukupende wewe kwa
sababu uumbaji upo ili kukutumikia wewe. Jua, mwezi, nyota, mvua, hewa, nchi,
miti, wanyama, samaki n.k, viko ili kukutumikia wewe.
Kama unafuga wanyama na wanakufa inamaana kuwa wanakuchukia.
Ustawi maana yake ni wewe kufikia kiwango ambacho uumbaji
unakupenda wewe.
Kumbu kumbu 28:1-2
“Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya
maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu
ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata
usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.” Itakuwa
inamaana gani? Maana yake ni pale utakapofikia kilele cha maisha yako; Unapo
zungumzia hatima maana yake umefika eneo la ukamilifu katika maisha yako.
Ukifikia kileleni ndipo sasa unaanza maisha bora na ndiyo yanaitwa ukamilifu.
“Itakuwa utakaposikia
sauti ya Bwana,” Ukifanya kile ulicho ambiwa ndipo sasa jambo litatokea
kwako.
Utakapo tii sauti ya Bwana Mungu wako ndipo unaweza kufikia
kilele cha mlima wako maana yake sasa umehitimu ki-maisha na ndipo kunakuwa na
thawabu kwa sababu umefanya kile ulichoambiwa. Ustawi ni thawabu ambayo
unaipata katika maisha baada ya kutimiza ule wajibu wako. Ukifika kileleni hiki
ndicho kinatokea kwao lakini kama sivyo utaishi kwa kung’ang’ana, kupambana na
utakuwa na uhitaji.
Tatizo sio vitu bali ni wewe haujafikia eneo ambalo Mungu
amekuitia uwe.
Kumbu kumbu 28:2 “Na
baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.” Wewe
haujui hizo Baraka zilipo lakini Mungu anajua ziko wapi, ukifikia kileleni mwa
mlimwa wako Baraka ndio zitakutafuta na si wewe unazitafuta.
Ukifikia kilele cha wito wako hauombi pesa wala chakula bali
unakuwa umepewa kila kitu, haupiganii kuishi bali kuna mtu anakuwa nakupigania.
Kufikia kileleni ni utukufu na ndio maana Yesu akasema; Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi
watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao
wamwabudu.” hii inamaana kuwa waabuduo halisi wapo kileleni na kwa sababu
hiyo wanasababisha pesa, watu n.k, wawakaribie au viwakaribie wao kwa sababu
wanavutia.
Kwa nini unang’ang’ana katika maisha yako leo? kwa sababu
haujafikia kilele cha wito wako, wito wako si kufukuza mapepo au kuponya
wagonjwa, la! bali wito ambao tumeitawa ni kumtumaini na kumpendeza Mungu;
ukifikia kipindi hicho ndipo utampendeza Mungu na Mungu anawatafuta watu kama
hao. Watu ambao wamefikia kiwango hicho hawaombi chochote kwa Mungu bali Mungu
anawaambia wafanye nini ili waweze kupata thawabu yao.
Ayubu 1:1 “Palikuwa
na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa
mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.” Huu
ndio ukamilifu, Ayubu aliwezaje kuwa mtu mkamilifu? Alikuwa mwelekefu, nini
maana ya uelekevu?
·
“Mwelekevu” Alipenda kujifunza kujua lipi baya na lipi jema.
·
“Aliyemcha Mungu” Ayubu alikuwa akimcha Mungu yaani alijitoa kwa
matumizi ya Mungu.
·
“Kuepukana na uovu.”Ayubu alikaa mbali na uovu.
Kwa sababu ya hayo ndipo Mungu alimpa Ayubu kustawi.
Ustawi ni thawabu hauupiganii, kuna watu wanafanya kazi kwa
bidii sana wakitumia nguvu nyingi na kuchoka lakini hawapati kitu chochote,
lakini watu wengine wanastawi kila iitwapo leo hata wasipofanya kazi ngumu, kwa
nini? Kwa sababu wamefika kilele cha mlima wao.
Uliumbwa kutimiza kile ambacho Mungu alitaka utimize na sio kile
ambacho wewe unataka kukitimiza, Mungu alituumba sisi ili kumfanya yeye awe
jinsi alivyo ili kwamba uumbaji wote lazima usalimu kwake, hii ndiyo sababu ya
uumbaji.
Mungu hakukuumba ili utimize mapenzi yako mwenyewe, la! Bali
kupitia wewe mapenzi ya Mungu yatimizwe. Wakati mwingine tunafanya mapenzi yetu
na kufikili kuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu, lakini sio kweli kwa sababu kama
ni kweli unatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yako hauwezi kuwa masikini.
Ayubu alipoteza kila kitu kwa muda wa miaka mitatu na baada ya hapo Mungu
akamrejeshea kila kitu, kwa nini kwa sababu aliamua kutimiza mapenzi ya Mungu
katika maisha yake.
Hatufungi ili vitu viende vizuri bali tunafunga ili sisi
tuendelee vizuri.
Usifunge ili kuifanya biashara yako iende vizuri bali Funga kwa
sababu unataka kufanya vizuri kwa Mungu wako ili biashara, pesa, wateja
wakufuate.
Tunafunga ili tuondoke katika kuchelewa na kurejea katika reli
yetu ili tuweze kwenda haraka na kufikia kule ambapo tunapaswa kuwa. Mtume Paulo
akasema Wafilipi 3:14 “nakaza
mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.” mwito
gani? Mwito wa ukamilifu ili kwamba lolote utakalo tenda upate kustawi na hapa
ndipo ustawi unapoanza.
Chochote utendacho kitastawi, kwa nini? Kwa sababu umeufikia
wito wako, hauwezi kustawi kama haujaufikia wito wako, bali utastawi baada ya
kuufikia mwito wako.
Mwito mkuu ni kwa wale ambao wamestawi; Usifunge ili duka lako
lichanue, wala usifunge na kuomba kwa sababu unataka kupanda cheo kazini, la
wewe funga na kuomba ili uungamanike na wito wako.
Daniel na wenzake hawakuomba ili wapande cheo, hapana! Bali
walifunga na kuomba ili wajiungamanishe na wito wao na kitu gani kilitokea?
Walichukuliwa katika kiwango cha heshima katika ule ufalme.
Kila mtu anawito wake jiungamanishe na wito wako na ujitoe kwa
Bwana wa mabwana ndipo utakuwa umeshinda.
Ustawi ni kwa ajili ya kila mmoja, ustawi unaenda na mtu ambaye
tayari anaufahamu wa kile alicho umbiwa.
Kila mmoja wetu anaweza kufanya maisha yawe bora ikiwa ukifahamu
maana ya ustawi. Watu wanaangalia sana vitu, wewe angalia wito wako ili uweze
kustawi.
Kama unataka kukaa katika mstari wako kuelekea wito wako unaweza
kuendelea kufunga mpaka usikie sauti ya Bwnaa.
Yohana 14:13 “Nanyi
mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya
Mwana.” Unapo chanua anayepewa utukufu ni Mungu wa Minguni na si wewe,
kwa nini? Kwa sababu Mbingu itasema ulicho kiumba kimetimiliza kile ambacho
umekiumbia. Utakapo fikia ustawi mbingu itamsifu Mungu na ibilisi pia.
Mungu anapenda kuwastawisha watu kwa maana anapo wastawisha si
kwa ajili yao bali ni kwa ajili yake mwenyewe lakini yeye anazo kanuni za
kuwastawisha watu.
Watu wengi ni masikini kwa sababu wanafikili kile walichonacho
ndio kinaweza kuwafanya wawe matajiri, lakini ukweli ni kuwa soi kweli. Pesa
inaweza ikakuelezea wewe ni nani, kama ni masikini au tajiri. Mara zote pesa
inapenda kwenda mahali ambapo tajiri yupo, utajiri sio pesa bali ni tabia, na
maisha ya ustawi ni thawabu.
Kama mtu anatabia ya utajiri mahali popote pale utakapo mpeleka
bila kumpa chochote lakini baada ya muda mfupi atakuwa tajiri, utajiri si pesa
bali ni tabia, je! Wewe unatabia gani?.
Kumbu kumbu 28:3 “Utabarikiwa
mjini, utabarikiwa na mashambani.” Baraka
sio pesa wala mahali bali ni tabia ya mtu; kama umebarikiwa basi umebarikiwa
hata uende wapi utabarikiwa, ukiwa unatembea na wito wako hauhitaji pesa ili
ubarikiwe bali Baraka zinapaswa kukufuata.
Acha wito wako utokee na kukuendesha ili kukufikia kilele cha
wito wako utafurahia.
Wale wote ambao mmefunga mwezi wa tano na mkamaliza, mkabarikiwe
na kustawi katika kila eneo la maisha yenu.
Ukastawi katika ndoa
yako, ibada yako, utajiri wako, ukastawi na katika kila eneo la maisha yako
likastawi kwa Jina la Yesu. Mungu akubariki.
Maoni