Agano la kale na Agano jipya

 



Mungu alifanya Agano mara mbili,

• Agano la Kale; Agano hili ni Agano la siku ambayo Mungu aliagana na Musa.

• Agano Jipya; Agano hili ni la Damu ambalo Mungu alilifanya na Yesu.

Lakini Biblia inasema Utukufu wa mwisho utakuwa mkubwa kuliko ule wa kwanza.

Malango ya kuzimu yalikuwa na nguvu juu ya Agano la siku yaani Agano la Kale, Agano la Kwanza lilitembea katika laana lakini Agano la Pili lilitembea katika Nguvu ya Mungu hivyo malango ya kuzimu hayana nguvu ya kulishinda.

Agano la Kwanza mtu alikuwa akiwa na mapepo anapigwa mawe mpaka afe, lakini Agano Jipya mtu akiwa na pepo anaombewa na huyo pepo anatoka. Agano la Kwanza lilikuwa katika siku lakini Agano la Pili hakuna Agano juu ya siku bali tunakumbuka yale yaliyotokea (matukio), hii ina maana kuwa tulihama kutoka katika siku na kuwa katika tendo.

Baada ya kuhama kutoka katika siku na kuingia katika tendo, hii ndiyo lilikuwa ni kumhalalisha mtu kuwa bwana wa siku yake, tendo hilo lilimuondoa mtu kutoka katika kuadhimisha siku na kuifanya hiyo siku imuazimishe yeye.

Agano Jipya limemuondoa mtu kunako siku na kumpeleka kunako Majira yake yaani Yeye ndiye anayeamrisha Siku na siyo siku inamuamrisha mtu kuwa ale nini au avae nini bali mtu anaiamrisha.

Mazingira yasikuamrishe wewe bali wewe yaamrishe, hali ya hewa isikuambie leo hii utanikoma bali wewe ndiyo uihamrishe, mbu asikuambie kuwa leo nitakulaza bali wewe ndiyo unamuamrisha akae mbali na wewe. Kutoka 25:16 “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.”

Agano Jipya limebadilisha siku yako na imekupa Mamlaka ya Kuiamrisha siku yako iendeje. Siku isikutengenezee wewe namna ya kuishi bali wewe ndiye unayepaswa kuitengenezea namna ya kufanya, lakini kwa nini siku inakuamrisha? Ni kwa sababu ya dhambi, dhambi ndiyo imekufikisha mahali pa siku kukuamrisha.

Unahangaika na maisha na kukopa hatimaye unaishia kuwa na madeni kila kona kwa sababu ya nini? Dhambi!, kwa sababu hiyo umeshindwa kuimiliki siku yako.

Ukiwa na uelewa Agano la Kale lilifanya nini na Agano Jipya lilifanya nini umeshinda, na kwa kupitia uelewa huo chochote unachokitaka katika Maisha yako kitatimia, hata ikifika mahali unasema kujenga nyumba unajenga siyo kwa sababu unapesa bali kwa sababu umetaka; yaani siyo siku yako inakuamrisha bali wewe ndiye unayeiamrisha

Agano la Kale lipo ili kukuonesha ni jinsi gani wewe ni mwenye dhambi, lakini Agano Jipya lipo ili kukuonesha ni jinsi gani wewe ni wa thamani machoni pa Mungu.

Dhambi ni nini? Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.” Dhambi ni kutokuwa na Ufahamu wa Mungu katika ufahamu wako; kulewa, kuzini, umaskini, kuacha au kuachwa kwenda kwa waganga, n.k, haya ni matokeo ya kutokuwa na uwelewa wa Mungu katika ufahamu wako.

Chochote unacho kihitaji kipo huku duniani; Mungu alituumba kwa sura yake na mfano wake lakini hivyo vyote viliondoka kwa mwanadamu baada ya dhambi na vimerudi kwetu baada ya kumwagika damu ya Yesu. Kila mmoja anayetambua nafasi ya Yesu au aliye na Ufahamu wa Yesu katika akili yake anarudishiwa hiyo nafasi ya kuwa kama Mungu.

Ndani ya ufahamu wa mtu alipewa mambo matatu makubwa na hayo ndiyo ibilisi aliyachukua na kwa hayo yalimfanya Yesu kuja duniani na akafa kwa ajili ya hayo.

1. Uzalishaji; Mwanzo 1:28 “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Ndani ya kila mmoja wetu aliumbiwa uzalishaji, kwa nini hauwezi kuzalisha leo hii? Kwa sababu uliharibiwa na dhambi ili kuirejesha hiyo inahitaji damu ya Yesu ili ikusafishe na dhambi. Haya yakisha tokea ndipo sasa wewe unaweza kuiamrisha siku yako.

2. Umiliki; Vitu vyote Mungu aliviumba lakini Yeye alitukabidhi sisi wanadamu ili tupate kuvimiliki, kama wewe umeolewa inamaana kuwa wewe ni mtawala wa mumeo, ukiona mume wako amechukuliwa na mwanamke mwingine ujue wewe mke umeshindwa kumiliki hivyo usimlaumu Mungu bali kaa kwenye nafasi yako, kazi ya kumbusu mume wako ni ya kwako sio ya Mungu ukishindwa kufanya hivyo akichukuliwa usimlaumu Mungu. Vile vile kazi ya kumtunza mke na kumfanya apendeze ni ya mwanaume, ukishindwa kumfanya mke wako apendeze wewe sio kichwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU