Kuongozwa na Roho.
Kuongozwa
na Roho.
Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila
mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:-
1.
Afanye kazi,
2.
Awe na umiliki juu ya nchi,
3.
Azalishe,
4.
Aombe,
5.
Ashuhudie,
6.
Aabudu,
7.
Lazima awe mtoaji,
8.
Lazima uwe na upendo, penda uumbaji,
9.
Lazima asamehe na atubu,
10. Ahakikishe
anatunza wito wake.
Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda,
1 Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza
yote, hata mafumbo ya Mungu.”
Mungu ametupa ufunuo
kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini,
maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo kuhusu wewe, Mungu au ya ibilisi
yaliyo katika roho hiki ndicho tunakiita ufunuo inamaana yamefunuliwa kwako.
Biblia inasema “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza
yote, hata mafumbo ya Mungu.” Hii inamaana kuwa Mungu
amekujulisha au amekusaidia kujua mambo yake kupitia roho. Unapo gundua mambo
ya Mungu yale yaliyofichwa na usiyoyajua yanaweza kuwa mazuri au mabaya makubwa
au madogo lakini Mungu amekujulisha kupitia roho huo ndio unaitwa ufunuo.
1 Wakorintho 2:11 “Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila
roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna
ayafahamuye ila Roho wa Mungu.”
Hakuna aujuaye moyo wako
kwa sababu ni wa kwako, chochote kilicho cha kwako ambacho hakijawahi
kufunuliwa kwa wengine inamaana ni cha kwako na anayekijua ni wewe mwenyewe.
Hakuna anayekujua wewe
kuliko unavyojijua mwenyewe sasa acha kuwawazia watu kwa maana wewe ndiye unaye
jijua mwenyewe, unakuta mtu anabeba vitu vingi kuhusu watu lakini Biblia
inasema hakuna ayafahamuye mambo ya wanadamu pasipo yeye mwenyewe, jitazame
wewe.
Ukitaka kufahamu mambo ya
Mungu kuwa wewe na uwe halisi, ukiwaza na kugundua mambo kuhusu wewe na
kutendea kazi mambo yako,kwa kufanya hivyo ndivyo unafungulia vitu kukujilia,
kwa nini wewe haupokei vitu kutoka kwa Mungu? ni kwa sababu unazingatia sana
kuhusu watu wengine na sio wewe.
Huwezi kumfahamu Mungu na
uumbaji wake, nia, matendo, nguvu, enzi na siri zake isipokuwa kupitia kwa Roho
wa Mungu.
1 Wakorintho 2:12 “ Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye
kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” Je!
Wewe umepokea roho gani; ya dunia au ya Mungu?.
Roho wa Mungu alikuja
kwetu ili kutufunulia, kutufungulia, kutuonyesha, kutuelekeza, kutuongoza na
kutushauri ni jinsi gani tunaweza kufikia mahali pa kuvipata vitu kutoka kwa
Mungu.
Daniel alitaka kumuona
Mungu na nguvu zake, uweza wake na kibali chake katika nchi ya ugenini, hivyo
roho wa Mungu alileta Mashauri ndani ya moyo wa Daniel. Daniel 1:10-13 “Mkuu wa matowashi akamwambia Danielii, Mimi namwogopa bwana
wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini
azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa
kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme……”
Daniel alipata mashauri
kutoka kwa roho wa Mungu kuwa asile chakula cha mfalme bali ale chakula cha
aina fulani kwa muda fulani. Unapo sikiliza moyo wako na ukimuomba Roho
Mtakatifu akuelekeze Yeye atakuongoza na utajua nini ufanye na kwa wakati gani.
Daniel 1:17 “Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na
ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote,
na ndoto.” Kwa sababu ya Daniel kusikiliza mashauri ya Mungu ya jinsi
gani ya kushughulikia mambo katika nchi ya ugenini, roho alimuelekeza Daniel na
ndipo Mungu akampa Daniel Maarifa na ujuzi katika elimu.
Daniel na wenzake
hawakwenda shule lakini Mungu aliwapa maarifa, ukiwa na Roho wa Mungu hauhitaji
kwenda chuo kikuu ili uwe na Ufahamu bali yeye atakupa ufahamu utokao kwa Mungu
na hakuna kitu kitakacho kushinda.
Daniel 2:15 “Hata mwisho
wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa
imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.”
Unapo sikiliza mashauri
unayopewa ndivyo unavyokuwa bora kuliko wenzako, Daniel na wenzake walikubali
kuongozwa na Roho na wakaamua kuyasikiliza mashauri yake na akawafanya kuwa
bora kuliko wengine.
·
Kwa nini upo hivyo ulivyo
leo? Ni kwa sababu hausikilizi mashauri unayopewa, unakuta mtu
anakwenda kanisani anafundishwa na kupewa mashauri lakini akitoka hafanyii kazi
kile alicho fundishwa.
·
Unakuta mtu ni mzuri sana kuhudhuria kanisani kila jumapili au
semina lakini yupo hivyo hivyo miaka yote, kwa nini? Kwa sababu hafanyii kazi
kile anacho fundishwa, halafu anasema yupo na Mungu, la! usijidanganye jua kuwa
uko wewe mwenyewe hauko na Bwana wa mabwana. Kama upo na Bwana wa mabwana na
unatendea kazi mafundisho yake unayopewa na watumishi wake kamwe hayo
mafundisho hayata kuacha uwe kama ulivyo bali yatakubadilisha.
Unachukuaje mambo ya
rohoni na kuyaleta katika ulimwengu huu wa kawaida,? Kwa kukubali kukitendea
kazi kile ulicho kisikia yaani mafundisho unayopewa.
1 Wakorintho 2:13 ” Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya
kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa
maneno ya rohoni.” Watu wanao tamani kukaa katika roho wanasikia mafundisho na
kamwe hawatakuwa wa kawaida, kwa nini? Kwa sababu wanasikiliza mafundisho
katika roho na wanafanyia kazi kiroho yale wanayo yasikiliza.
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye
kuwahesabia haki.” 38-39 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala
mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala
yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala
kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika
Kristo Yesu Bwana wetu.”
Mimi kupitia Pendo la
Kristo Yesu nipo hapa nilipo, kutoka kutokuwa na jina mpaka utele; yote haya ni
kutokana na Pendo la Kristo ndani yangu. Hii ndio maana anasema yeyote aliye
ndani ya pendo la Yesu anakuwa ni kiumbe kipya.
Kama kweli wewe umeokoka
inamaana kuwa umekuwa kiumbe kipya kwa maana hiyo hakuna cha kukutenga na pendo
la Kristo Yesu, kwa sababu kupitia hilo Pendo linakufanya uwe mshirika wa mambo
ya Mungu katika roho ndani ya Kristo Yesu.
Waefeso 1:3-4 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki
kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama
vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe
watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.”
Ukiwa katika roho utakuwa
na uwezo wa kuingia katika roho kupitia roho yako na kuchukua yale ambayo
umekirimiwa na kuyaleta katika maisha haya ya kawaida, hivyo kamwe hautakuwa
masikini.
Maoni