Mauya aliuota ushindi vs Simba
Mauya aliuota ushindi vs Simba
MONDAY JULY 05 2021
BAADA ya kuwalaza na viatu Simba juzi kwenye mechi ya derby, mfungaji pekee wa bao la Yanga, Zawadi Mauya amefunguka kuwa alijua wanaenda kushinda mchezo huo hata kabla ya mechi kuanza.
Mauya ambaye ni kiungo mkabaji ilimchukua dakika 11 tu kuiandikia Yanga bao la kuongoza na la ushindi baada ya kupiga shuti kali akiwa nje ya boksi la 18 lililoenda wavuni baada ya kumgonga Shomari Kapombe wa Simba na kubadili mwelekeo wakati kipa Aisha Manula akiwa amesharukia upande huo kuufuata.
Mauya alisema kuwa yeye na wachezaji wenzake walijua kuwa watapata ushindi kutokana na ubora wa timu yao na maandalizi waliyoyafanya.
“Tuliingia uwanjani tukijua tunashinda, mimi na wachezaji wenzangu kabla ya mchezo huu tulijiwekea mikakati ya kushinda mechi hii hivyo ilikuwa lazima tushinde.
“Lile bao nililifunga kutokana na kutumia vyema nafasi niliyopata, nilifurahi sana kufunga na kikubwa zaidi nimefurahi kuipatia timu ushindi kwenye mechi kubwa kama hii,” alisema Mauya.
Maoni