Siku 100 za Rais Samia Suluhu: Kibarua kilichopo mbele serikali ya kudhibiti corona

 

Siku 100 za Rais Samia Suluhu: Kibarua kilichopo mbele serikali ya kudhibiti corona

  • 05julai  2021
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum ya corona kutoka kwa Profesa Said Aboud.

 picha, Ikulu, Tanzania

Maelezo ya picha,

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum ya corona kutoka kwa Profesa Said Aboud.

Ripoti iliyozinduliwa na kamati maalum ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu COVID-19, bila shaka imeiweka nchi hiyo katika ramani ya dunia kuhusu maswala ya usalama wa afya ulimwenguni. Hata hivyo, kwa kuzingatia hali ilivyo kwa sasa nchini humo, serikali inakabiliwa na jukumu zito la kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya wanasayansi.

Changamoto iliyowazi kwa sasa ni kuwepo kwa mkanganyiko mkubwa kijamii na kisaikolojia uliochagizwa na utata wa mbinu zilizotumika dhidi janga la COVID-19 wakati wa utawala wa hayati Rais John Magufuli. Tofauti na ilivyo sasa, ukweli uko kwenye rekodi kwamba utawala uliopita haukuwa wazi kuhusu kuwepo kwa janga nchini licha ya viongozi wa dini na wanaharakati kupaza sauti juu ya uwepo wa maambukizi na vifo.

Kukana uwepo wa janga kwa muda mrefu au kupuuza athari zake kumeathiri mitazamo ya jamii kwa kiasi kikubwa. Pia kumezalisha tatizo la ziada katika jitihada za mamlaka za afya nchini humo kwenye kutekeleza mapendekezo ya wanasayansi kuhusu kujilinda dhidi ya tishio la wimbi la tatu la COVID-19. Kunahitajika hatua za haraka ili kukabiliana na hali hii, kabla hata ya kutekeleza hatua nyingine zaidi, mathalani kuanzisha huduma za chanjo.

Mapendekezo ya kamati kwa serikali yamekuja wakati ambapo mamlaka za afya tayari zilikuwa zimetoa tahadhari juu ya janga hilo na ikiwa safari za ndege kwenda India zimesimamishwa na hatua zaidi za ukaguzi katika viwanja vya ndege zikiwa zimeongezwa. Pia, uamuzi wa rais kuongoza kwa mfano kwa kuvaa barakoa hadharani umeongeza ari katika kupambana dhidi na uwezekano wa janga kutokea tana nchini humo.

Inavyoonekana, viongozi waandamizi katika serikali ya Rais Samia wameiga mfano na kuanza kuvaa barakoa, tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma. Hata hivyo, hii ni ishara tu kwamba walau kuna utashi wa kisiasa katika kukabiliana na janga hilo.

Kazi iliyopo mbele ni kuishawishi jamii ambayo mitazamo yake na mazoea yao juu ya hatua za kujikinga, kama kuvaa barakoa na fikra zao juu ya chanjo viliathiriwa na mitazamo na maamuzi ya utawala uliopita wa hayati Rais Magufuli pamoja na sababu nyingine.

Upinzani au uasi katika sayansi?

Kwa muda murefu katika utawala uliopita, sayansi na imani hasi juu ya COVID-19 vilipata nafasi kubwa nchini Tanzania bila kudhibitiwa. Jamii kutoelewa mienendo ya wanasayansi pia kumeongeza mkanganyiko. Vipande vya video au sauti vimesambaa sana katika mitandao ya kijamii vikinukuu watafiti au watu wenye ushahidi hasi juu ya chanjo ya COVID-19 na mambo mengine kadhaa.

Rais Samia

Ni muhimu kufahamu kwamba katika kutafiti ukweli kuhusu COVID-19 ni kawaida kabisa kuwepo kwa mawazo kinzani miongoni mwa wanasayansi. Hii ni kwa sababu sayansi hutegemea maafikiano baina ya wanasayansi. Lakini wapo baadhi ya wanasayansi ambao huamua kwenda kinyume na ushahidi wa kisayansi uliokubaliwa kwa ujumla. Kwa mfano, hadi leo hii wapo wanasayansi wasioamini kwamba kirusi cha HIV ndicho husababisha UKIMWI. Hawa huitwa wanasayansi waasi au kwa kiingereza; science dissidents. Mawazo yao ni muhimu kuyaheshimu tu.

Mara nyingi, wanasayansi waasi huwa na ushahidi hafifu kuhusu kile wanachokitetea na kwa maana hiyo hukosa fursa au vigezo vya vya kuchapisha maandiko yao katika majarida ya kisayansi. Mwishowe huamua kuwasilisha ushahidi wao kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari. Jamii inaweza kuwaamini watu hawa nakujikuta katika mkanganyiko mkubwa. Jambo hili lina madhara makubwa katika afya ya jamii kama mamlaka za za afya hazitoi elimu sahihi kuhusu sayansi iliyo sahihi na iliyokubaliwa au kuthibitishwa kwa ujumla.

Mkanganyiko ulipozaliwa

Afua za kisayansi dhidi ya COVID-19 ziliingiliwa na mitazamo ya kisiasa na kidini nchini Tanzania tangu Aprili 8 mwaka jana (2020) wakati viongozi mashuhuri serikalini na viongozi kadhaa wa dini na wanasiasa walipoanza kupenyeza maoni ambayo ni kinyume na makubaliano ya jumla ya kitafiti juu ya sayansi ya COVID -19.

Nimefuatilia kwa ukaribu majadiliano ya umma kwenyevyombo vya habari na mitandao yakijamii nchini Tanzania. Pia, mimefanya mahojiano na watu wa kawaida. Nilichobaini nikwamba yale maoni ya wanasiasa kuhusu COVID-19, mfano "Korona ni shetani "au" "ni vita ya kiuchumi, "au "Chanjo si salama" bado fikra hizi ziko hai na huenda zikawa zimekita mizizi katika jamii.

Hayati Rais John Magufuli
Maelezo ya picha,

Hayati Rais John Magufuli alikosolewa vikali kwa namna alivyopambana na virusi vya corona.

Kwa miezi mingi iliyopita tangu mwaka jana, wanasayansi wa Tanzania hawakuwa na nafasi ya kutosha kuelimisha jamii juu ya sayansi yenye uthibitisho kuhusu kirusi cha korona na ugonjwa. Umma uliachwa katika mkanganyiko, huku serikali ikitoa taarifa za kutatanisha kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa virusi nchini humo. Kwa sasa, taifa limegawanyika sana katika wanaounga mkono au wanaopinga ukweli wa kisayansi kuhusu njia za kuzuia COVID-19, pamoja na chanjo.

Ni rahisi kwa nadharia zenye utata kupenya kwa urahisi katika jamii iliyogawanyika. Hii inatokea hata katika nchi zingine. Lakini pia, kulingana na takwimu za Wizara ya Afyan chini Tanzania, asilimia kati ya 70 hadi 80 ya watu huamini katika uponyaji wa jadi au tiba asili.

Hiyo inaweza pia kudokeza ni kwa nini zaidi ya miaka 10 iliyopita, wagonjwa kadhaa waliripotiwa kukimbia hospitali na wengine walikataa dawa zao za kisasa wakati maelfu walipomiminika nyumbani kwa mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile au Babu wa Lolidondo ambaye alidai Mungu alimpa maono juu ya dawa ya asili ambayo "huponya" saratani, ugonjwa wa sukari na shinikizo la juu la damu.

Kwa hali ilivvyo hivi sasa, endapo ukifanywa utafiti leo kwa kufuatilia maoni ya watu, mitazamo na mienendo yao juu ya hatua za kinga kama vile kuvaa barakoa na matumizi ya chanjo nchini Tanzania, matokeo yanaweza kuonesha jinsi mitazamo hasi ilivyokita mizizi.

Na hii ndiyo hatua inayopaswa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa hivi sasa. Kutokana na mitazamo mbalimbali hasi kuhusu mbinu za kisayansi za kujikinga na COVID-19, hatari itokanayo na ugonjwa huu inaweza kuwa inachukuliwa kwa wepesi sana.

Katika hali kama hiyo, utekelezaji wa afua za mapema dhidi ya tishio la wimbi la tatu, kama ilivyopendekezwa na kamati ya Rais, utakuwa na kibarua kigumu hapo mbeleni. Yawezekana kabisa watu wakawa wanafikiri kwamba nilazima kuonekane ongezeko la vifo katika jamii ndipo waanze kuchukua tahadhari. Maamuzi kama haya yanagharama yake.

Kwa bahati mbaya, wakati ongezeko la vifo linaanza kuonekana katika jamii, maambukizo kawaida huwa yamefikia katika hatua ambayo ni vigumu kukabiliana nayo. Wimbi la pili lilipokuwa katika kilele chake katikati ya mwezi wa Februari, ndipo watu walipoanza kuchukua tahadhari. Hali kama hiyo, ni hatari.

Jamii yetu iondolewe kwenye dimbwi la mkanganyiko

Kampeni ya elimu kwa umma inahitajika ili kubadili mtazamao wa jamii.


Maelezo ya picha,

Kampeni ya elimu kwa umma inahitajika ili kubadili mtazamao wa jamii.

Hatua ya hivi karibuni ya Rais Samia kuonekana akichukua tahadhari kwa kuvaa barakoa na kushawishi viongozi wote wa umma kufanya hivyo ni hatua nzuri katika mwelekeo sahihi. Inatuma ujumbe mzuri ambao unaweza kuleta mabadiliko katika tabia miongoni mwa jamii. Lakini je, inatosha?

Kabla ya kitu kingine chochote, ni muhimu kampeni thabiti ya elimu kwa umma izinduliwe ili kuondoa mkanganyiko na imani potofu zilizojikitika katika jamii juu yaCOVID-19 na chanjo.

Kinachoweza kuokoa umma kwa sasa ni ujumbe wa elimu kwa umma ambao sio lazima upingane na imani zilizojikita miongoni mwa umma na siyo lazima kuhubiri kwamba sayansi ya chanjo ya COVID-19 inafaa, bali kusisitiza juu yalengo la kulinda maisha na kuepuka athari zitokanazo na ugonjwa, hasa pale unaposambaa zaidi nchini bila hatua thabiti kuchukuliwa. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU