Tanzania kutengeneza chanjo yake ya corona

 

Tanzania kutengeneza chanjo yake ya corona

Tanzania imeanza mchakato wa kutengeneza chanjo yake ya virusi vya corona ili kupunguza gharama ya kuagiza chanjo hiyo nje ya nchi.

Taarifa ya Serikali iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wa nchi hiyo, Profesa Abel Makubi imesema chanjo hiyo itatengenezwa kupitia kiwanda chake kipya ambacho kipo kwenye mchakato wa kuanzishwa.

Prof. Makubi hata hivyo hakueleza mchakato huo ambao umesharidhiwa na Rais Samia Suluhu Hassan upo katika hatua gani hasa na lini kiwanda kinatarajiwa kukamilika na kuanza kuzalisha chanjo.

Mpaka sasa hakuna nchi ya Afrika iliyoanza kutengeneza chanjo ya Corona, ingawa nchi za Uganda, Rwanda, Afrika Kusini na Senegal zilitangaza kuanza mipango ya kutengeza chanjo. Haifahamiki pia endapo Tanzania itashirikiana na nchi nyengine ama mashirika ya kimataifaCopyright: Wizara ya Afya Tanzania/ TwitterImage caption: Profesa Abel Makubi imesema chanjo ya corona itatengenezwa kupitia kiwanda kipya

Tanzania inasema imechukua uamuzi huo kwa kuwa ina wataalamu waliobobea wa chanjo: "tuna wataalamu wakutosha kwa hiyo tunataka huo mchakato wa kuanza kutengeza chanjo zetu sio tu kwa ajili ya Covid-19 pekee yake, hata chanjo zingine hiki kiwanda kitaweza kuzalisha ili kupunguza gharama, lakini pia kuzifanya ziwe karibu na wananchi’, alisema Makubi siku ya Jumapili akiwa Dodoma.

Mbali na hilo nchi hiyo pia imetoa mwongozo mpya wa kukabiliana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona shuleni. Miongoni mwa mambo yaliyopitishwa wakati shule zikifunguliwa hii leo nchini humo ni;

  • Walimu, wafanyakazi na wakufunzi kuvaa barakoa wakati wote wakiwa shuleni.
  • Wanafunzi kuvaa barakao wakati wote wakiwa darasani.
  • Na uwepo wa vifaa vya kunawia mikono, kuwekea taka na kutoewa kwa elimu kuhusu virusi hivyo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Rais Samia, nchi hiyo ambayo kwa zaidi ya mwaka mmoja ilikuwa haijatangaza takwimu za ugonjwa huo ina wagonjwa zaidi ya 100 wa Corona, 70 wakiwa kwenye mitungo ya oksijeni.

Wakati huo huo, Tanzania tayari imeshatuma maombi ya kujiunga na mpango wa chanjo wa Covax kama ilivyoshauriwa na Kamati ya Wataalamu iliyoundwa na rais Samia kumshauri juu ya namna ya kukabiliana na janga la corona.

Mpango wa Covax ambao moja ya waratibu wake ni Shirika la Afya Duniani (WHO) unalenga kuhakikisha nchi masikini ulimwenguni zinapata chanjo hizo muhimu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU