Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 13.07.2021
Manchester United wako mbioni kukubaliana masharti binafsi na mlinzi wa Real Madrid Raphael Varane,27, ambaye amekuwa akitolewa macho kwa muda mrefu.(Daily Mail)
Hector Bellerin ameiambia Arsenal kuwa anataka kuondoka wakati wa dirisha la usajili majira ya joto. Mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi mwenye miaka 26, ambaye ni mchezaji wa muda mrefu wa kikosi cha kwanza cha Mikel Arteta ana matumaini ya kuhamia Inter Milan. (Metro)

Manchester City haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Antoine Griezmann, 30, lakini wana nia na mshambuliaji wa Norway na Borussia Dotmund Erling Braut Haaland, 20, na nahodha wa Tottenham England Harry Kane. (The Sun)
Chelsea inatarajia kutangaza 'ofa kubwa' kwa Haaland. (Daily Star)

Griezman anaweza kuelekea kwenye klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid, kwa kubadilishana na kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez,26. (Daily Express)
Tweet ya kiungo wa kati wa Real Madrid Isco -iliyofutwa - inadokeza kwamba mchezaji huyo wa Uhispania ataondoka wakati wa miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake kuisha, huku Arsenal, Tottenham Hotspur na Napoli wakimtolea macho. (Daily Mirror)
Manchester City na Wolverhampton Wanderers zote ziko katika mipango ya kumnasa mlinzi wa Fulham mwenye umri wa miaka 23 Antonee Robinson.(Daily Mirror)
Juventus wanamlenga mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, 24. Klabu hiyo ya Italia pia imemuorodhesha mshambuliaji wa Everton Muitaliano Moise Kean, 21. (Tuttosport, via Daily Mail)

Arsenal inaelekea ukingoni kumnasa kiungo mchezeshaji wa Lyon Houssem Aouar, 23 na kiungo wa kati Mbelgiji Albert Sambi Lokonga, 21, anayekipiga Anderlecht. Pia kiungo wa kati wa Leicester City James Maddison, 24, yuko kwenye mipango ya Arsenal. (The Sun)
Kocha mpya wa Crystal Palace, Patrick Vieira anampanga mlinda mlango wa Kiingereza Remi Matthews, 27, ambaye ameachiliwa tu na League one ya Sunderland. (Daiily Mirror)
Maoni