Unayajua matokeo ya kushangaza zaidi kwenye historia ya mashindano haya?
Euro 2020: Unayajua matokeo ya kushangaza zaidi kwenye historia ya mashindano haya?
Tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 60 iliyopita, Michuano ya Euro imekuwa na matokeo yasiyotabirika na ya kushangaza, kuanzia ubingwa walioupata Denmark na Ugiriki mpaka ushujaa usiotarajiwa wa Iceland.
BBC inakuletea matokeo 10 ya kushangaza katika historia ya michuano hiyo, ambapo matokeo ya hivi karibuni kabisa ni ya kwenye mashindano ya Euro 2016. Katika mashindano ya mwaka 2016 ambapo timu zilizoonekana kama vibonde zilizoa karibu asilimia 29 ya mechi zote zilizozaa ushindi, ikiwemo ushindi iliyoupata Ureno katika mechi ya fainali dhidi ya Ufaransa.
Wakati mashindano ya Euro yakienda kuanza wiki hii, kwa kushirikiana na wataalamu wa data, Gracenote tunakueletea kumbukubu za kushangaza za mashindano haya yenye umaarufu mkubwa duniani na kushirikisha wachezaji wakubwa wa soka duniani.
10. England 0-1 Yugoslavia - (Nusu fainali - Euro 1968)
Wakitoka kutwaa ubingwa wa kombe la dunia miaka miwili nyuma, England wanaingia uwanjani kweye mchezo wa fainali kwenye mashindano ya Euro mwaka 1968 nchini Italia, wanakutana na kipigo cha kushangaza kutoka kwa vibonde, Yugoslavia ambao walipewa nafasi ya ushindi ya asilimia 21.9. Kikosi cha kocha, Alf Ramsey kikiwa na nyota kama Bobby Moore, Bobby Charlton, Gordon Banks na Geoff Hurst kilijawa na matumaini ya kutwaa kombe lingine kubwa, lakini alikuwa Dragan Dzajic aliyemtungua Banks katika dakika ya 86 na kuzima matumaini na ndoto zote za England.
Mabingwa watetezi Ujerumani Magharibi walihitaji alama moja tu ili waweze kufuzu hatua ya nusu fainali kama washindi wa pili wa kundi lao, lakini walikwaa kisiki cha Hispania wakati huo ilikuwa timu ya kawaida ikipewa 21.7% ya nafasi ya ushindi.
Goli la Antonio Maceda katika dakika ya mwisho ya mchezo, inawarudisha nyumbani Ujerumani Magharibi iliyokuwa chini ya Jupp Derwall, na kuwaacha Hispania kuongoza kundi lao kabla ya kwenda kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa.
8. Ureno 1-2 Ugiriki - (Mechi ya makundi - Euro 2004)
Kama kuna mashidano ambayo yalijaa maajabu, basi ni haya ya Euro 2004. Ushindi wa Ugiriki katika mechi ya fainali dhidi ya Ugriki, unatajwa kama ushindi wa kushangaza zaidi katika historia ya mashindano hayo. Ugiriki ilipewa 24.5% ya nafasi ya kushinda mchezo huo.
Ugiriki walishawashangaza Wareno iliyokuwa chini ya Kocha Luiz Felipe Scolari tangu mchezo wa kwanza katika makundi, baada ya kuwachapa 2-1 kwa magoli ya Georgios Karagounis na Angelos Basinas, goli la kufutia machozi la Ureno lilifungwa na Cristiano Ronaldo. Hakuna aliyetarajia matokeo haya.
7. Ukraine 0-2 Ireland Kaskazini- (Mechi ya Makudi -Euro 2016)
'Matokeo haya sidhani kama yanaweza kujirudia tena katika miaka 30 ama 40 ijayo'. Haya yalikuwa maneno ya Nial McGinn miaka minne baadae baada ya kufunga goli la kukumbukwa katika Euro 2016. Ireland Kaskazini ilipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Ukraine, goli lingine likifungwa kwa kichwa na Gareth McAuley. Ulikuwa ushindi wa kwanza wa Ireland Kaskazini kuupata katika mashindano makubwa, ushindi ambao ulitosha kukipeleka kikosi cha Michael O'nell kwenye hatua ya mtoano.
6. CIS 0-3 Scotland - (Mechi ya Makundi - Euro 1992)
"Leo mkiingia uwanjani, mtakuwa mmefanya kitu ambacho hakuna mchezaji yeyote wa Scotland aliyewahi kufanya,"maneno ya Kocha wa Scotland, Andy Roxburgh kwa wachezaji wake muda mfupi kabla ushiriki wao wa mara ya kwanza kwenye mashindano ya Euro mwaka 1992.
Baada ya kuchapwa na Uholanzi na Ujerumani katika mechi mbili za kwanza, Scotland ilitolewa, lakini ikapata ushindi wa kushangazi katika mechi ya mwisho ya kundi lake, dhidi ya Commonwealth of Independent States (CIS) - iliyoundwa kufuatia muungano wa Soviet.
Paul McStay, Brian McClair na Gary McAllister waliisaidia Scotland kupata ushindi huo mnono wa mabao 3-0 na kuondoka kwenye mashindano haya kishujaa.
5. Uholanzi 0-1 Denmark - (Mechi ya Makundi - Euro 2012)
"Tunaweza kusema, tunaionea wivu timu ya Uholanzi, tungetamani kuvaa viatu vyao, wanapewa nafasi kubwa, hakuna shaka kwenye hilo." Yalikua maneno ya kocha wa Denmark , Morten Olsen wakati huo, na hata kocha wa Uholanzi yenyewe, Bert van Marwijk alikiri kwamba walipewa nafasi kubwa katika Mashindano ya Euro 2012, ingawa awali ilionekana kama mchezo wa kuchezeana akili.
Uholanzi, wakitoka kushika nafasi ya pili kwenye kombe la duinia miaka miwili nyuma, wanashangazwa na kichapo kutoka kwa Denmark kupitia mkwaju wa kipindi cha kwanza wa Michael Krohn-Dehli, mbaya zaidi wakapoteza michezo yote mitatu ya mashindano hayo na kutolewa kwenye mashindano. Hata hivyo kwa Denmark licha ya ushindi huo wa ajabu walishindwa kusonga mbele kwenye hatua ya mtoano.
4. Ubelgiji 0-2 Uturuki - (Hatua ya Makundi - Euro 2000)
"Hii ni zawadi kwa Uturuki nzima," Kocha wa Uturuki, Mustafa Denizli alisema. "Haya ni mafanikio makubwa katika miaka 77 ya historia ya soa la Uturuki."
Furaha ya Denizli ilifuatia ushindi wa Uturuki wa mabao 2-0 dhidi ya Ubelgiji katika Euro 2000, na kuifanya Uturuki kufuzu hatua ya makundi katika mashindano makubwa kwa mara ya kwanza kabisa na kuiondoa Ubelgiji iliyokuwa mwenyeji mwenza wa mashindano hayo.
Hakan Sukur alifunga mabao yote mawili ya vibonde hao waliopewa 19.7% ya nafasi ya kushinda, ambao katika mechi mbili za awali walipata alama moja tu.
3. Ubelgiji 1-3 Wales - (Robo fainali - Euro 2016)
'Kama ningekuwa mwenyekiti wa klabu ya Ligi kuu England ningemsajili Hal Robson-Kanu," alisema mshambuliaji wa Wales, John Hartson.
Ni usiku wa kukumbukwa katika historia ya mpira ya Wales na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ubelgiji ukafanya kuwa matokeo ya ajabu ya tatu katika mashindano ya Euro. Goli zuri la Robson-Kanu kama lilivyoelezwa na Hartson - linasherehesha ushindi wa kukumbukwa katika Euro 2016.
Ikishiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano makubwa kwa karibu miaka 58, kikosi cha Chris Coleman, kilitoka nyuma na kuichapa Ubelgiji 3-1 na kufuzu nusu fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
Radja Nainggolan aliitanguliza Ubelgiji kwa mkwaju wa umbali wa mita 25 yards, lakini magoli ya Ashley Williams, Robson-Kanu - ambaye wakati huo hakuwa na klabu na goli la Sam Vokes yalibadili matokeo.
2. France 0-1 Greece - (Robo fainali - Euro 2004)
Ni wakati mzuri katika historia ya soka la Ugiriki," Alisema Angelos Charisteas, mfungaji pekee wa goli la Ugiriki katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Ufaransa. Kwa wakati huo maneno yake yalikuwa yana maana, ambapo kikosi cha Otto Rehhagel kilifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2004 kwa kuwaondosha wenyeji Ufaransa.
Les Blues walishindwa kusawazisha bao la kipindi cha pili la kichwa la Charisteasr licha ya kuwa na nyota kama Zinedine Zidane, Robert Pires na Thierry Henry.
Lakini maneno ya Charisteas hayakuchukua muda, kwani Ugiriki iliendelea kupata matokeo ya kushangaza kwa kuichapa Czech Republic bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali kabla ya kuibwaga Ureno nyumbani mjini Lisbon na kutwaa kombe lake la kwanza kabisa katika mashindano makubwa.
1. England 1-2 Iceland - (16 bora -Euro 2016)
"Ni sie tu tuliokuwa tunaaamini inawezekana. Dunia nzima haikuwa inaamini, lakini sisi tuliamini."Haya yalikuwa maoni ya beki Kari Arnason, baada ya yeye na wachezaji wenzake wa Iceland kuweka rekodi ya matokeo ya kushangaza zaidi kwenye historia ya mashindano hayo. Huenda kipigo hicho kikawa kipigo cha aibu cha England kuwahi kupokea katika mashindano yoyote yale.
Kipigo hicho kimeelezewa na mshambuliaji wa zamani wa England Alan Shearer kama "mchezo mbovu kabisa kuuona wa England ". Iceland ilitoka nyuma na kuichapa England 2-1 katika mchezo wa 16 bora wa Euro 2016.
Goli la penati la dakika ya nne la Wayne Rooney ilionyesha kama ungekuwa mchezo mwepesi kwa kikosi cha England, lakini Ragnar Sigurdsson na Kolbeinn Sigthorsson walibadili matokeo ndani ya dakika 14, matokeo ambayo yalimfanya kocha wa England, Roy Hodgson kujiuzulu. Yalikuwa matokeo ya kushangaza zaidi.
Maoni