KUONGOZWA NA ROHO.

 
 KUONGOZWA NA ROHO.
Maombi ni lazima, tumehimizwa na muumbaji kuomba, Kwa kila mwamini anapaswa kuwa na mambo yafuatayo:-
1.      Afanye kazi,
2.      Awe na umiliki juu ya nchi,
3.      Azalishe,
4.      Aombe,
5.      Ashuhudie,
6.      Aabudu,
7.      Lazima awe mtoaji,
8.      Lazima uwe na upendo, penda uumbaji,
9.      Lazima asamehe na atubu,
10.  Ahakikishe anatunza wito wake.
 
Ukiyaweka haya pamoja ndipo unakuwa yule ambaye Mungu anampenda,
 
1 Wakorintho 2:10 “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
Mungu ametupa ufunuo kupitia roho wake, ufunuo ni nini? Maana yake ni kugundua mambo yaliyo sirini, maswala ya kiroho ukiyagundua yale yanayo kuhusu wewe, Mungu au ya ibilisi yaliyo katika roho hiki ndicho tunakiita ufunuo inamaana yamefunuliwa kwako.
Biblia inasema “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” Hii inamaana kuwa Mungu amekujulisha au amekusaidia kujua mambo yake kupitia roho. Unapo gundua mambo ya Mungu yale yaliyofichwa na usiyoyajua yanaweza kuwa mazuri au mabaya makubwa au madogo lakini Mungu amekujulisha kupitia roho huo ndio unaitwa ufunuo.
 
1 Wakorintho 2:11 “Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
 
Hakuna aujuaye moyo wako kwa sababu ni wa kwako, chochote kilicho cha kwako ambacho hakijawahi kufunuliwa kwa wengine inamaana ni cha kwako na anayekijua ni wewe mwenyewe.
Hakuna anayekujua wewe kuliko unavyojijua mwenyewe sasa acha kuwawazia watu kwa maana wewe ndiye unaye jijua mwenyewe, unakuta mtu anabeba vitu vingi kuhusu watu lakini Biblia inasema hakuna ayafahamuye mambo ya wanadamu pasipo yeye mwenyewe, jitazame wewe.
Ukitaka kufahamu mambo ya Mungu kuwa wewe na uwe halisi, ukiwaza na kugundua mambo kuhusu wewe na kutendea kazi mambo yako,kwa kufanya hivyo ndivyo unafungulia vitu kukujilia, kwa nini wewe haupokei vitu kutoka kwa Mungu? ni kwa sababu unazingatia sana kuhusu watu wengine na sio wewe.
 
Huwezi kumfahamu Mungu na uumbaji wake, nia, matendo, nguvu, enzi na siri zake isipokuwa kupitia kwa Roho wa Mungu.
1 Wakorintho 2:12 “ Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” Je! Wewe umepokea roho gani; ya dunia au ya Mungu?.
 
Roho wa Mungu alikuja kwetu ili kutufunulia, kutufungulia, kutuonyesha, kutuelekeza, kutuongoza na kutushauri ni jinsi gani tunaweza kufikia mahali pa kuvipata vitu kutoka kwa Mungu.
Daniel alitaka kumuona Mungu na nguvu zake, uweza wake na kibali chake katika nchi ya ugenini, hivyo roho wa Mungu alileta Mashauri ndani ya moyo wa Daniel. Daniel 1:10-13 “Mkuu wa matowashi akamwambia Danielii, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme……
Daniel alipata mashauri kutoka kwa roho wa Mungu kuwa asile chakula cha mfalme bali ale chakula cha aina fulani kwa muda fulani. Unapo sikiliza moyo wako na ukimuomba Roho Mtakatifu akuelekeze Yeye atakuongoza na utajua nini ufanye na kwa wakati gani.
Daniel 1:17 “Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.” Kwa sababu ya Daniel kusikiliza mashauri ya Mungu ya jinsi gani ya kushughulikia mambo katika nchi ya ugenini, roho alimuelekeza Daniel na ndipo Mungu akampa Daniel Maarifa na ujuzi katika elimu.
Daniel na wenzake hawakwenda shule lakini Mungu aliwapa maarifa, ukiwa na Roho wa Mungu hauhitaji kwenda chuo kikuu ili uwe na Ufahamu bali yeye atakupa ufahamu utokao kwa Mungu na hakuna kitu kitakacho kushinda.
 
Daniel 2:15 “Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.”
Unapo sikiliza mashauri unayopewa ndivyo unavyokuwa bora kuliko wenzako, Daniel na wenzake walikubali kuongozwa na Roho na wakaamua kuyasikiliza mashauri yake na akawafanya kuwa bora kuliko wengine.
·         Kwa nini upo hivyo ulivyo leo? Ni kwa sababu hausikilizi mashauri unayopewa, unakuta mtu anakwenda kanisani anafundishwa na kupewa mashauri lakini akitoka hafanyii kazi kile alicho fundishwa.
·         Unakuta mtu ni mzuri sana kuhudhuria kanisani kila jumapili au semina lakini yupo hivyo hivyo miaka yote, kwa nini? Kwa sababu hafanyii kazi kile anacho fundishwa, halafu anasema yupo na Mungu, la! usijidanganye jua kuwa uko wewe mwenyewe hauko na Bwana wa mabwana. Kama upo na Bwana wa mabwana na unatendea kazi mafundisho yake unayopewa na watumishi wake kamwe hayo mafundisho hayata kuacha uwe kama ulivyo bali yatakubadilisha.
Unachukuaje mambo ya rohoni na kuyaleta katika ulimwengu huu wa kawaida,? Kwa kukubali kukitendea kazi kile ulicho kisikia yaani mafundisho unayopewa.
1 Wakorintho 2:13 ” Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.” Watu wanao tamani kukaa katika roho wanasikia mafundisho na kamwe hawatakuwa wa kawaida, kwa nini? Kwa sababu wanasikiliza mafundisho katika roho na wanafanyia kazi kiroho yale wanayo yasikiliza.
Warumi 8:33 “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.” 38-39 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Mimi kupitia Pendo la Kristo Yesu nipo hapa nilipo, kutoka kutokuwa na jina mpaka utele; yote haya ni kutokana na Pendo la Kristo ndani yangu. Hii ndio maana anasema yeyote aliye ndani ya pendo la Yesu anakuwa ni kiumbe kipya.
 
Kama kweli wewe umeokoka inamaana kuwa umekuwa kiumbe kipya kwa maana hiyo hakuna cha kukutenga na pendo la Kristo Yesu, kwa sababu kupitia hilo Pendo linakufanya uwe mshirika wa mambo ya Mungu katika roho ndani ya Kristo Yesu.
Waefeso 1:3-4 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Ukiwa katika roho utakuwa na uwezo wa kuingia katika roho kupitia roho yako na kuchukua yale ambayo umekirimiwa na kuyaleta katika maisha haya ya kawaida, hivyo kamwe hautakuwa masikini.

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMSHINDA SHETANI

NGUVU YA DAMU YA YESU

VIPAJI VYA ROHO MTAKATIFU