Mungu akitokea kwako kama mfalme ana sehemu zake nne.
Mungu
akitokea kwako kama mfalme ana sehemu zake nne.
1. Mshauri, Ukifikia hatua hii ndiyo wakati huu kitu cha kwako kinakuwa cha kwake na cha kwake kinakuwa cha kwako. Hivyo huwezi kukubali kuona Matakatifu ya Mungu yanachafuliwa ndivyo hasira ya Mungu inawaka juu yako, kuna watu wanakasirika wakisengenywa wao lakini wachungaji au viongozi wao akisengenywa unaona kawaida, jifunze kuyalinda matakatifu ya Mungu hata kama yatakughalimu. Mungu ana njia nyingi za kuwapa watu wake unatakiwa uwe na wivu wa Mungu.
2. Mungu mwenye nguvu, Lengo lakujionyesha ni kukufanya uweze kufika kwenye kufanya miujiza na pia kupokea miujiza na pia uweze kufanya yale ambayo ulikuwa huwezi kufanya ana maana gani? Anamaanisha atakupa usaidizi kwa sababu wewe ni raia wake.
3. Baba wa
milele, ili kukupa wewe urithi wako, kukufanya urithi, yamkini baba yako hana
chochote au alishakufa, unachotakiwa kujua yupo Baba wa mbinguni ambaye Yeye
atakupa urithi wako. neno baba maana yake ni kujali, sasa utajuaje Inaonekana
katika Zaburi 23 unauona ubaba, pia zaburi 91 unauona ubaba, Zaburi 128 unaona
ubaba pale, Warumi 8:28 unauona ubaba pale Waefeso 3:20 unauona ubaba pale.
Utakaposoma vizuri na ukutamka utayaona mambo yakitokea kwako.
Wazazi
ndiyo watu pekee ambao wanaweza kukufanyia jambo na likaonekana au akafanya
jambo pasipo wewe kumuomba, hivyo ukimchukulia Mungu kama Baba hiki ndicho
utakipata kwenye maisha yako.
Unapoenda mbele za Mungu kumuomba chakula au mahitaji maengine kama mwenye haki inawezekana usiyapate mahitaji yako kutokana na makosa uliyoyafanya kabla kuomba, bali ukimuomba kama Baba utapata chakula kwa sababu baba humpa chakula mwanae hata kama amefanya makosa.
4. Mfalme wa amani, pale panapokuwa na maadui wengi, vikwazo vingi, pale ambao milango imefungwa unamuhuitaji mfalme wa amani. Ni wakati gani unamuhitaji mfalme wa amani? Ni pale ambapo unataka kustawi ili akufariji, kwa sababu amani ikiwepo ndani yako itakufanya utende mema, ukikosa amani ndani yako lazima utatapeliwa, ukikosa amani ndani usiende kufanya jambo lolote linalohusu biashara n.k. Hata kama unataka kuchumbia usiende kuchumbia kama huna amani hutompata, hata kama kuna mchumba amekuja na ndani yako hakuna amani usikubali maana ataishia kukudanganya tu.
Amani ni nini? Amani inakwenda sawasawa na neno uhakika wa jambo, yaani ukishaona unaamani na hilo jambo maana yake unauhakika na hilo jambo, imani ni Yesu lakini amani ni Mungu, kwahiyo amani siyo yako bali ni ya Mungu, ndiyo maana neno linasema “Amani ya Bwana iwemo mioyoni mwenu” ndipo akasema MFALME WA AMANI. Ukishakuwa na amani hakuna jambo lolote litakalo kushinda.
Ukishafikia
mahali pa wewe kuwa na amani hakuna kitu kitakachokushinda kama una amani na
kicheko kimejaa kila jambo kwako litakuwa sawa, kama unataka kuwa na fedha na
afya njema hakikisha amani haiondoki ndani yako, ndiyo maana neno linasema
“kuwa na amani na watu wote” hivyo huwezi kuyaona ya Mungu kama hutakuwa na
amani.
Ili uweze
kuchanua ni lazima uwe na amani lakini hiyo amani huwezi kuipata kama mfalme wa
amani hayuko na wewe.
Katika yote ili uweze kufikia mambo haya manne tabia yako lazima ibadilike kwa sababu tabia yako ndiyo itakayokufanya ukutane na kile unachokitamani.
Kila tabia
mbaya iliyo ndani yako hakikisha unairekebisha kwa kuwa usipoirekebisha
Mbinguni hutaenda, haijalishi wewe ni mtoto wa nani. Usipobadili tabia yako
mbaya, utaiona hii Dunia ni chungu na utaona Mbinguni ni mbali.
Kataa
tabia zote ambazo Mungu amezikataza ili usishindwe kuingia kwenye Uzima wa
Milele. Siku zote hakikisha Yesu yupo moyoni mwako maana anapokuwa ndani yako
hutajiongoza mwenyewe bali utaongozwa na Yeye siku zote.
Usichoke
kumngoja Bwana, hata kama maombi yako hayajajibiwa. Neno linasema,
"Wamngojao Bwana hawataaibika".
Kanisa la
leo wengi hawana subira; Ndio maana unamkuta mtu ameokoka halafu bado anaenda
kwa mganga. Waganga wengine wameamua kutumia jina la Yesu wakijua watu wataenda
tu kwa sababu wanapenda njia ya mkato, zidi kumngoja Bwana Yesu kwa uaminifu
wote naye atajitokeza kwako.
Maoni